• Nairobi
  • Last Updated December 4th, 2023 6:37 PM
Kizaazaa demu akimpokonya polisi bunduki ndani ya lojing’i

Kizaazaa demu akimpokonya polisi bunduki ndani ya lojing’i

NA MWANGI MUIRURI

KARATINA, NYERI

KULIZUKA kizaazaa katika lojing’i moja ya mji huu afisa wa polisi alipopokonywa bunduki yake na kahaba katika mzozo wa malipo.

Afisa huyo alikuwa amefika katika baa moja iliyoko karibu na steji kuu na katika hali ya kula raha baada ya kupokea mshahara, akaamua kuchukua kipusa wa bei.

“Walikuwa wamekubaliana bei ya Sh500 waburudishane kwa angalau saa moja, lakini haieleweki afisa huyo alishikwa na hisia gani kwa kuwa dakika chache baadaye, kulisikika fujo kutoka chumbani,” akasema bawabu wa eneo hilo.

Kwa kuwa baa hiyo huwa imejaa makahaba, kulizuka mtafaruku mkuu huku wenzake mwanamke huyo wakijitokeza katika chumba hicho kutuliza hali.

“Cha kushangaza ni kwamba kahaba huyo alikuwa amekatalia bunduki ndogo ya afisa huyo akitisha kumfyatulia risasi ikiwa hangelipa pesa jinsi walivyokuwa wamekubaliana,” meneja wa baa hiyo akadokeza.

Afisa huyo naye alikuwa akitisha kumkabili mwanamke huyo kama jambazi aliyekuwa akijaribu kuiba bunduki ambayo ni mali ya serikali.

“Unajua vizuri kuna msako wa wanaohatarisha uthabiti wa serikali iliyoko madarakani… Hapa tuliko ni ngome ya naibu wa kiongozi wa nchi. Haiwezekani ujaribu kutwaa bunduki ya serikali na nikuache tu hivyo,” afisa mlevi mnunuzi wa mahaba akafoka.

Lakini waliokuwa hapo walimkumbusha kwamba hakuwa kwa kazi ya serikali wakati huo bali alikuwa katika soko la mahaba akiwa mlevi na pia uchi.

“Ndipo alifichua kwamba mwanamke huyo alikataa kujifaragua ili warushane roho na pia hakuwa akitaka watumie mipira ya kondomu. Baada ya mwanamke kukataa, akasema hangeshiriki biashara hiyo na ndipo kukazuka purukushani hiyo, mwanamke akinyakua bunduki ya afisa kama fidia,” akasema bawabu.

Mambo yalisuluhishwa baada ya meneja kutisha kumwita mkubwa wa usalama eneo hilo ili aje asuluhishe mzozo huo.

“Afisa aliamua kulipa hata ikiwa alilalamika sana wote waliokuwa hapo walifanya muungano wa kumnyanyasa lakini akalipa kupitia huduma ya simu,” akasema meneja.

  • Tags

You can share this post!

IPOA inajikokota kuchunguza polisi walioua raia –...

Kocha wa Soccer Assassins atuma onyo kwa Solasa

T L