• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 6:07 PM
Huzuni tele ajuza waliouawa kwa madai ya uchawi wakizikwa

Huzuni tele ajuza waliouawa kwa madai ya uchawi wakizikwa

Na WYCLIFFE NYABERI

WINGU la simanzi lilikigubika kijiji cha Nyagonyi, eneo la Marani, Kaunti ya Kisii wakati wa mazishi ya ajuza watatu walioteketezwa kwa tuhuma za uchawi wiki tatu zilizopita.

Kauli za “Viva! Viva! Haki Kwa Wakongwe wa Marani na Sote Tuko Tayari Dhuluma Zikija” ndizo zilizokuwa kauli mbiu za maafisa kutoka kwa Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu (KNCHR).

Kila aliyepata nafasi ya kuhutubu alikemea kitendo hicho cha kinyama kilichosikitisha Wakenya na kulaani waliotenda maovu hayo.

Viongozi wa makanisa kutoka madhehebu mbali mbali, pamoja na viongozi wa serikali ya Kaunti ya Kisii, walikemea na kusema walisikitishwa na hali ya binadamu kuingiwa na unyama.

Wanamuziki wa bendi tofauti zinazoimba nyimbo kwa lugha ya Ekegusii, walitunga wimbo wa kukemea uozo ambao umekithiri katika jamii.

Jamaa wa ajuza hao waliolemewa na hisia, walibubujikwa na machozi wakiwa wamebeba picha za akina mama hao.

You can share this post!

Mahakama yaokoa spika katika meno ya madiwani

DINI: Katika hali zote zinazokupata kumbuka kila kitu...

T L