• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 8:11 PM
Kaunti za Mulembe zilitumia mabilioni kwa ziara – Ripoti

Kaunti za Mulembe zilitumia mabilioni kwa ziara – Ripoti

Na DERICK LUVEGA

KAUNTI nne za Magharibi mwa Kenya, kwa jumla zilitumia Sh1.2 bilioni kwa ziara za humu nchini wakati wa janga la corona, Mwelekezi wa Bajeti (COB) amefichua katika ripoti ya mwaka wa kifedha wa 2020/21.

Hiki ndicho kipindi ambacho nchi hii ilikuwa ikikabiliana na athari za janga la corona ambalo lilivuruga uchumi, na kusababisha mapato ya sekta zote kudidimia.

Ripoti ya Mwelekezi wa Bajeti inaonyesha kuwa kaunti za Vihiga, Bungoma, Busia na Kakamega kwa jumla zilitumia Sh27.2 milioni kwa ziara za nje ya nchi katika kipindi hicho.

Ripoti hiyo inaonyesha kwamba Kaunti ya Bungoma iliongoza kwa matumizi ya ziara hizo kwa Sh429.5 milioni, ikifuatiwa na Vihiga iliyotumia Sh303.7 milioni.

Kaunti za Kakamega na Busia zilitumia Sh280.4 milioni na Sh208.5 milioni kwa ziara za humu nchini mtawalia.

Vihiga haikutumia pesa zozote kwa ziara za nje ya nchi katika mwaka wa kifedha wa 2020/21.

Hata hivyo, Kaunti ya Kakamega ndiyo iliyotumia kiasi cha chini cha pesa kwa ziara za ng’ambo ikiwa ni Sh696,855. Bungoma inaongoza kwa kutumia Sh14.1 milioni ikifuatwa na Busia iliyotumia Sh12. 4 milioni kwa ziara nje.

Kulingana na ripoti, hii ilifanya matumizi ya ziara za humu nchini kuzidi matumizi mengine huku mapato yakipungua na kuzifanya kutegemea mgao kutoka serikali kuu pekee.

You can share this post!

Wazee watangaza kuhubiri amani 2022

Kamishna aamuru ukaguzi kuzuia bidhaa za magendo kutoka...

T L