• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 9:48 PM
Korti yabatilisha uamuzi kuhusu bondi ya Sh300,000

Korti yabatilisha uamuzi kuhusu bondi ya Sh300,000

NA JOSEPH WANGUI

MAHAKAMA Kuu imebatilisha uamuzi wa mahakama ya chini ulioamuru kufutiliwa mbali kwa dhamana ya Sh300,000 pesa taslimu dhidi ya mchezaji raga wa zamani, Alex Olaba katika kesi ya ubakaji.

Dhamana hiyo ilitupiliwa mbali mnamo Mei 2021 kufuatia madai kwamba, Bw Olaba alikula njama za kumuua shahidi mmoja wa upande wa mashtaka katika kesi hiyo.Jaji Grace Nzioka, hata hivyo, amebatilisha uamuzi wa hakimu baada ya kubaini kuwa, hatua ya kufutilia mbali dhamana hiyo haikufuata utaratibu ufaao.

Kwenye uamuzi wake katika kesi iliyowasilishwa na wakili wa Bw Olaba, Cliff Oduk, korti ilibaini kuwa mshukiwa alihukumiwa bila kupatiwa fursa ya kusikilizwa.

“Mawasilisho mapya yamekubalika na dhamana imerejeshwa. Mshukiwa hakusikizwa kabla ya uamuzi,” ilisema korti.

Aidha, ilibainika kwamba mawasilisho rasmi hayakutolewa kabla ya kufutilia mbali dhamana wala kuwasilishwa kwa nakala ya kiapo na afisa anayechunguza kesi hiyo ili kuthibitisha madai yaliyotolewa dhidi ya Bw Olaba kuhusu njama za mauaji.

Kufuatia hatua hiyo, mchezaji raga huyo wa zamani wa Kenya Sevens alitupwa rumande katika Gereza la Industrial Area hadi kesi hiyo itakaposikizwa na uamuzi kutolewa.

  • Tags

You can share this post!

DARUBINI YA UKWELI: IEBC ndiyo hudhibiti Sajili ya...

Hafla ya Uhuru yakera maafisa wa Somalia

T L