• Nairobi
  • Last Updated June 15th, 2024 6:55 AM
Raia wa Uholanzi motoni kwa kudhulumu watoto kingono

Raia wa Uholanzi motoni kwa kudhulumu watoto kingono

NA RICHARD MUNGUTI

RAIA wa Uholanzi alishtakiwa Ijumaa, Desemba 8, 2023 kwa kuwadhulumu watoto wa umri wa miaka 16 na 17 kimapenzi katika kaunti ya Uasin Gishu kati ya 2022 na 2023.

Jan Int Veld almaarufu Dad Ok almaarufu Teacher Jan almaarufu Mzungu, alishtakiwa katika Mahakama ya kuamua kesi za watoto Milimani Nairobi.

Mzungu alikana mashtaka matano ya kuwadhulumu watoto hao kimapenzi alipofikishwa mbele ya hakimu mkazi Bi C C Oluoch.

Upande wa mashtaka ulipinga Mzungu kuachiliwa kwa dhamana ukisema “akiachiliwa atatoroka kwa vile adhabu ya mashtaka yanayomkabili ni kali”.

Mzungu aliagizwa azuiliwe katika gereza la Viwandani (Industrial Area) hadi Desemba 11, 2023.

Miongoni mwa mashtaka yanayomkabili ni pamoja na kuwaonyesha filamu za ngono watoto hao kwa nia ya kuwashawishi washiriki ngono naye.

Mzungu alishtakiwa siku 17 baada ya raia wa Amerika Terry Ray Krieger kushtakiwa katika mahakama ya Mavoko kwa kuwadhulumu kimapenzi watoto.

Krieger, mwenye umri wa miaka 68, aliyefungwa na mahakama ya Nairobi miaka 50 na kuachiliwa katika mazingira tata na Jaji Momanyi Bwonwong’a, aliyestaafu, amezuiliwa katika gerezani la Kitengela hadi Feburuaru 22, 2024 kesi itakapotengewa siku ya kusikizwa.

  • Tags

You can share this post!

Raila amtaka Ruto kushusha bei ya mafuta ya petroli kwa...

Wanaume Wamaasai sasa wakumbatia upangaji uzazi

T L