• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 10:50 AM
Shujaa kikaangoni ikilenga robo-fainali Vancouver 7s

Shujaa kikaangoni ikilenga robo-fainali Vancouver 7s

NA GEOFFREY ANENE

TIMU ya taifa ya raga ya Kenya Shujaa itavaana na Amerika, Fiji na Uingereza katika mechi kali za Kundi A kwenye Raga za Dunia duru ya Vancouver Sevens, Jumamosi.

Vijana wa kocha Innocent Simiyu walichapwa mara ya mwisho walikutana na wapinzani hao.Walibwagwa na Amerika 12-10 Jumamosi iliyopita, Fiji 19-5 Novemba 2021 na Uingereza 24-19 mnamo Januari 2020.Kibarua kigumu kinachosubiri Shujaa ni kuwa imepoteza dhidi ya Fiji mara saba mfululizo. Shujaa pia imelimwa na Fiji mara nne mfululizo nchini Canada ikiwemo 36-12 Machi 2019.

Kenya inashikilia nafasi ya 10 katika ligi hiyo ya mataifa 16, kwa jumla ya alama 36 baada ya duru za Dubai I, Dubai II, Malaga, Seville na Singapore. Kuna duru tisa msimu huu.

Vijana wa Simiyu wana ushindi mmoja dhidi ya Amerika katika mechi tano zilizopita, ingawa kila mmoja alichabanga mwenzake 24-19 wakati Canada ilikuwa mwenyeji msimu uliopita mijini Vancouver na Edmonton.Pia, Shujaa haina rekodi nzuri dhidi ya Uingereza ambapo imekung’utwa mara saba mfululizo, ingawa ilivuna ushindi wa 12-0 zilipokutana mara ya mwisho nchini Canada mwezi Machi 2018.

“Mchezo wetu ulikuwa wastani mjini Singapore. Juhudi zetu zilikosa uimara na tulifanya makosa makubwa wakati muhimu wa mechi yaliyotunyima alama. Lengo letu linasalia kufika robo-fainali katika duru ijayo (Vancouver Sevens),” Simiyu alieleza Taifa Leo.

Kenya inashikilia nafasi ya 10 katika ligi hiyo ya mataifa 16 kwa jumla ya alama 36 baada ya duru za Dubai I, Dubai II, Malaga, Seville na Singapore. Kuna duru tisa msimu huu. Herman Humwa na Billy Odhiambo ni baadhi ya wachezaji ambao wamekuwa wakifanya vyema Shujaa msimu huu.

  • Tags

You can share this post!

Raha muogeleaji Mkenya Kalombo akinyakua dhahabu Afrika...

Burnley wamtimua kocha Sean Dyche

T L