• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 3:55 PM
Wanawake wawili wafikishwa kortini kwa utapeli wa Sh15.6 milioni za watafutaji ajira

Wanawake wawili wafikishwa kortini kwa utapeli wa Sh15.6 milioni za watafutaji ajira

NA RICHARD MUNGUTI

WANAWAKE wawili waliokamatwa na polisi kwa kuwatapeli wasaka kazi 28 zaidi ya Sh15.6 milioni wakidai wamewatafutia kazi nchini Canada wameshtakiwa.

Kati ya Mei 2022 na Juni 2023 Lucy Nyokabi Kiutho na Staphristah Njeri Karani, hakimu mkuu mahakama ya Milimani Lucas Onyina, alifahamishwa wawili hao waliwalaghai watafutaji wa ajira kati ya Sh71,000 hadi Sh2 milioni.

Mahakama imeelezwa Nyokabi na Njeri waliwavutia wasaka kazi hao kwa kuwapa matumaini kwamba watawasafirisha hadi nchi hiyo ughaibuni na kuwapa kazi nzuri zitakazobadilisha maisha yao pamoja na watu wao.

Mahakama ilielezwa na kiongozi wa mashtaka Anderson Gikunda kwamba hapingi washtakiwa hao wakiachiliwa kwa dhamana ila alimsihi hakimu azingatie kitita kikubwa cha pesa ambacho wasaka kazi walitapeliwa na washtakiwa akiamua ombi lao la kuachiliwa kwa dhamana.

Washtakiwa hao waliomba mahakama iwaachilie kwa dhamana wakiahidi kutii masharti watakayopewa na korti.

“Dhamana ni haki ya kila mshtakiwa isipokuwa upande wa mashtaka uwasiliasha sababu mufti za kupinga wakiachiliwa huru wahudhurie kesi kutoka makwao,” wakili anayewatetea washtakiwa alimweleza hakimu.

Akitoa uamuzi, Onyina alisema hatawaachilia washtakiwa kwa dhamana hadi pale wawili hao watakapohojiwa na afisa wa urekebishaji tabia kubaini ikiwa washtakiwa hao wako na rekodi za kushiriki uhalifu hapo awali.

Punde tu baada ya kutoa uamuzi huo, washtakiwa hao Nyokabi na Njeri walipelekwa moja kwa moja hadi Gereza la Wanawake la Lang’ata hadi Juni 30, 2023 ripoti ya probesheni (urekebishaji tabia) itolewe.

Onyina aliweaeleza washtakiwa watakaohojiwa na afisa wa probesheni pamoja na wahasiriwa wa vitendo vyao kabla ya ripoti kuwasilishwa kortini.

Walalamishi katika kashfa ya kazi za ng’ambo wafanya mkutano nje ya mahakama baada hakimu Lucas Onyina kuamuru Lucy Nyokabi Kiutho na Njeri Karani kuamurwapelekwe gerezani hadi Juni 30, 2023 baada ya kukana kuwalaghai Sh15.6 milioni. PICHA | RICHARD MUNGUTI

Idadi kubwa ya wazazi na jamaa wa waliotapeliwa walifika kortini na kufanya mkutano nje ya mahakama kujadiliana hatua watakayochukua warudishiwe pesa zao.

“Hatuwezi poteza pesa na kazi. Lazima washtakiwa waturudishie pesa zetu kisha waadhibiwe kwa mujibu wa sheria,” mlalamishi mmoja katika kesi.

Aliagiza idara ya urekebishaji tabia iwahoji Nyokabi na Njeri wabainike ikiwa wako na rekodi za uhalifu za hapo awali kabla ya kuamua ikiwa wataachiliwa kwa dhamana au la.

Pia wahasiriwa wa ulaghai huo watahojiwa waeleze ikiwa wako na upingamizi washtakiwa wakiachiliwa kwa dhamana.

Nyokabi alikabiliwa na mashtaka 25 peke yake.

Wote wawili -Nyokabi na Njeri walishtakiwa pamoja kumlaghai Lawrence Karithi Banu Sh2 milioni kati ya Mei 27, 2022, na Mei 13, 2023 jijini Nairobi.

Kati ya Mei 18 na Juni 3, 2023, Nyokabi alishtakiwa kumlaghai Josephine Muthoni Njue Sh71,000 wakidai watampeleka Canada kazini.

  • Tags

You can share this post!

Nation FC yapangwa katika Kundi C michuano ya SJAK

Tottenham wajinasia kipa matata Guglielmo Vicario

T L