• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 6:07 PM
Wahadhiri, wahudumu wa vyuo vikuu vya umma watishia kugoma

Wahadhiri, wahudumu wa vyuo vikuu vya umma watishia kugoma

Na FAITH NYAMAI

WAHADHIRI na wafanyakazi wa vyuo vikuu vya umma wametishia kulemaza masomo katika taasisi za elimu ya juu ikiwa vyuo vikuu wanakofanya kazi havitawalipa malimbikizi ya mishahara yao.

Wakihutubia wanahabari jijini Nairobi jana, maafisa wa miungano mitatu ya vyuo vikuu vya umma, Muungano wa Watoaji Huduma katika Taasisi za Elimu (Uasu), Muungano wa Wafanyakazi katika Vyuo Vikuu Nchini (Kusu) na Muungano wa Wafanyakazi Nyumbani, Hotelini, Taasisi za Elimu na Hospitalini (Kudheiha) waliitaka serikali kuagiza vyuo vikuu kulipa malimbikizi ya pesa zilizosalia bila kuzichelewesha tena.

Aidha, miungano hiyo imeagiza kuwepo kituo kimoja cha kushughulikia mishahara katika vyuo vyote ili kuhakikisha wafanyakazi wote katika daraja moja ya kazi wanapata kiasi sawa cha mishahara katika vyuo vyote vikuu.Kupitia taarifa ya pamoja iliyosomwa na Katibu Mkuu wa Uasu Dkt Constantine Wasonga , wafanyakazi katika vyuo vikuu walishutumu taasisi za elimu ya juu dhidi ya kutekeleza kiholela Mkataba wa Malipo ya Mishahara wa 2017-2021 na kuwanyima wafanyakazi mishahara yao kamili.

Hii ni licha ya serikali kutoa Sh8.8 kwa vyuo vikuu kuhusu CBA ili kulipa mishahara ya waajiriwa. “Miungano haitapumzika hadi mikataba ya CBA ya 2017-2021 itakapotekelezwa kikamilifu na kama sivyo migomo ambayo tumekuwa nayo katika baadhi ya vyuo vikuu itaendelea,” alisema Dkt Wasonga.

Afisa huyo alisema jana kuwa kutokana na masuala ya vyuo vikuu, miungano kwa ushirikiano na Baraza la Vyuo Vikuu vya Umma (IPUCCF), taasisi inayosimamia vyuo vikuu, iliunda Kamati ya Utekelezaji Nchini (NIC) kuchunguza jinsi vyuo vikuu vinavyotekeleza mkataba wa CBA wa 2017-2021.

Ukaguzi huo ulifanywa kati ya Septemba 1 na Septemba 28, 2021.Dkt Wasonga alisema masuala makuu yaliyojitokeza katika utafiti wa NIC ni kuwa, mbinu ya utekelezaji wa CBA hapo mbeleni ilisababisha wafanyakazi kushushwa vyeo kwa kuwasogesha nyuma kwa miaka mitatu kwenye viwango vya chini zaidi vya mishahara.

You can share this post!

Mtaa kwenye mpaka hata polisi waogopa!

Chanjo ya kuzuia corona yaharibika

T L