• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
Biden akataa kutuma ndege za kivita nchini Ukraine

Biden akataa kutuma ndege za kivita nchini Ukraine

NA XINHUA

WASHINGTON, AMERIKA

RAIS wa Amerika, Joe Biden, amekataa kuidhinisha kutumwa kwa ndege za kivita za F-16 nchini Ukraine.

Biden alipinga uwezekano wowote wa kutuma ndege za kivita katika nchi hiyo.

“Hapana, hatutatuma ndege za kivita Ukraine,” akasema Biden alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kutuma ndege za kivita Ukraine.

Kadhalika, alieleza mpango wake wa kutembelea nchi ya Poland.

Matamshi hayo ya rais yamekuja huku mjadala ukizidi kuendelea kuhusu iwapo nchi hiyo itaipatia Ukraine silaha za kupambana na Urusi.

Alipoulizwa uamuzi wa serikali yake kuhusu uwezekano wa kuwasilisha F-16 kwa Ukraine, Naibu Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Amerika, Jonathan Finer, alisema kwamba “Amerika haijaamua”.

“Tumejaribu kuwasilisha usaidizi wetu kwa nchi ya Ukraine. Hata hivyo, hatujaamua ikiwa ndege hizo zitatumwa,” akasema Finer.

Ijapokuwa ni ombi la mara kwa mara kutoka kwa mamlaka ya nchi ya Ukraine, ndege za kivita kwa muda mrefu zinachukuliwa na Magharibi kama vifaa vinavyoweza kuzua mzozo zaidi usioweza kudhibitiwa.

Waziri wa Mambo ya Nje Ukraine, Dmytro Kuleba, alisema kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter Jumatano iliyopita kwamba kupata msaada ya ndege za kivita za aina hiyo kutoka Magharibi ni hatua muhimu.

Siku iyo hiyo, Amerika na Ujerumani zilitangaza maamuzi yao ya kutuma mizinga ya kivita nchini Ukraine. Ombi la Ukraine la kutaka ndege za kivita lilikataliwa na Ujerumani, ambayo Kansela wake, Olaf Scholz, hivi majuzi alisema ndege za kivita sio za maana kwenye orodha ya Berlin.

“Suala la ndege za kivita halijitokezi hata kidogo,” Scholz alisema katika mahojiano na Tagesspiegel.

“Tunachojaribu kuepuka ni kuingia katika shindano la kila mara la silaha za kivita,” akasema Scholz.

Mwaka 2022, Urusi ilitishia kuongeza mashambulio yake nchini Ukraine kufuatia mpango wake wa kuchukua makombora ya masafa marefu kutoka kwa mataifa ya magharibi.

“Iwapo makombora hayo yatapewa Ukraine, tutatumia silaha zetu kushambulia maeneo ambayo hatujawahi kulenga,” alisema Rais Vladimir Putin.

Putin alisema hatua ya mataifa ya magharibi kuipatia Ukraine silaha zaidi itachelewesha tu kumalizika kwa vita kati yake na Ukraine na kuzorotesha hali ya kibinadamu.

Tangu vita hivyo kuanza, wengi wamepoteza maisha na biashara kadhaa kuathiriwa.

  • Tags

You can share this post!

CHARLES WASONGA: Serikali iwachukulie hatua kali walimu...

Idadi ya waliokufa kwa bomu yafika 95

T L