• Nairobi
  • Last Updated November 28th, 2023 6:55 PM
Mambo yamechemka: Mulamwah, Ruth K watangaza wanatarajia mtoto pamoja

Mambo yamechemka: Mulamwah, Ruth K watangaza wanatarajia mtoto pamoja

NA FRIDAH OKACHI

MPENZI wa Mulamwah, Ruth K ameweka wazi kwamba anao ujauzito kutokana na picha ambayo ameiweka kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.

Mulamwah ambaye jina lake halisi ni David Oyando ni msanii na wakati mwingi amekuwa akimrejelea Ruth K kama bestie (yaani rafiki wa dhati).

Kwenye picha aliyopakia katika ukurasa wa Instagram na kudhihirisha ni mjauzito, Ruth K alisimulia jinsi alijipata na kuzama kwenye mapenzi.

Mwanadada huyo alisema matokeo  hayo, yalianza kama urafiki na kufuatwa na mapenzi na kuishia kuwa mjamzito kwa kiumbe kinachosubilriwa ma wengi wenye upendo.

Ruth K akiweka wazi ni mjamzito. Picha kwa hisani ya Instagram

Ruth K anatarajia kuitwa mama kwa kupata mwanawe ambaye ni kifungua mimba.

“Kwanza ilianza kwa upendo, upendo ambao uliumba maisha mapya, baraka ambayo hutujaza na furaha. Kutengeneza maisha ni hisia bora zaidi? yayari unapendwa. Natamani sana kukutana nawe,” Ruth K alisema.

Msanii Mulamwah alichangia kwenye chapisho hilo na kusema hali hiyo ni kutokana na mipango iliyoratibiwa na Mwenyezi Mungu. Vilevile aliweza kupakia picha ya mrembo huyo na ujumbe sawia na huo.

Bestie, Mungu alifanikisha,” Mulamwah aliandika.

Takribani mwezi mmoja uliopita, wawili hao walifanya sherehe ya kitamadnuni nyumbani ishara kuwa ni familia moja.

Mulamwah baadaye katika mahojiano na waandishi wa habari za mitandaoni, alikanusha kuwa haikuwa sherehe ya kuhusishwa na ndoa kwani alikwenda kwa kina Ruth K tu kuwasalimia kwa vile yeye pia alishawahi fika kwao.

Hata hivyo, msanii huyo amekuwa akikwepa kusema iwapo bestie ana ujauzito. Mulamwah amekuwa akisisitiza kinachoonekana ni vazi tu la Ruth K ambalo pengine fundi alikuwa amelishona vibaya kutokana na haraka ya kulishona.

  • Tags

You can share this post!

Mke ataka mume aliyemshambulia kwa panga na kumpa ulemavu...

Mama mkwe wa Maina Njenga azirai akilishwa kiapo kortini

T L