• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 3:46 PM
BORESHA AFYA: Fahamu ni kwa nini unafaa kunywa chai ya halwaridi

BORESHA AFYA: Fahamu ni kwa nini unafaa kunywa chai ya halwaridi

NA MARGARET MAINA

[email protected]

HALWARIDI ina historia ndefu ya kutumika katika upishi na ni ya kunukia.

Lakini pia inatumika kama dawa za kijadi.

Watu wengi hufurahia chai ya halwaridi kwa ladha yake, harufu, na manufaa yake kiafya.

Kihifadhi asili

Chai hii inaweza kusaidia kupambana na maambukizi. Majani ya halwaridi hutumiwa katika dawa za jadi kwa athari zake za kupigana na bakteria na uponyaji wa jeraha.

Inaweza kusaidia kupunguza sukari yako ya damu

Ikiwa haijatibiwa, sukari ya juu inaweza kuharibu macho, moyo, figo na mfumo wa neva. Kwa hivyo, ni muhimu kwamba watu walio na ugonjwa wa kisukari wadhibiti ipasavyo viwango vyao vya sukari ya damu.

Chai ya halwaridi inaweza kusaidia kupunguza sukari ya damu mwilini na kudhibiti sukari ya juu ya damu kwa watu wenye ugonjwa wa kisukari.

Inaweza kuboresha hisia zako na kumbukumbu

Kupitia dhiki na wasiwasi mara kwa mara ni jambo la kawaida.Kunywa chai ya halwaidi kunaweza kusaidia kuongeza hisia zako na kuboresha kumbukumbu yako.

Harufu ya halwaridi inaonekana kuwa ya manufaa. Kuvuta pumzi yenye harufu ya halwaridi kunaweza kuboresha umakini, utendaji na hisia.

Inaweza kusaidia afya ya ubongo

Misombo katika chai ya halwaridi inaweza kulinda afya ya ubongo wako kwa kuzuia kifo cha seli za ubongo.

Halwaridi pia inaweza kuzuia athari mbaya za kuzeeka kwa ubongo. Ndiyo hata maana inapendekezwa kama kinga dhidi ya magonjwa ya mfumo wa neva kama vile Alzheimer’s.

Inaweza kulinda afya ya maono na macho

Kuongeza dondoo ya halwaridi kwenye tiba za aina nyinginezo kama kumeza dawa kunaweza kupunguza kasi ya kuendelea kwa magonjwa ya macho yanayohusiana na umri.

  • Tags

You can share this post!

Vita vya tatu bora KWPL ikiingia raundi ya 11

Kisura anayelenga kupata mavuno mazuri katika uigizaji

T L