• Nairobi
  • Last Updated March 5th, 2024 5:55 AM
Mbunge Milly Odhiambo atumai hata yeye atapata mtoto uzeeni kama yule nyanya wa Uganda

Mbunge Milly Odhiambo atumai hata yeye atapata mtoto uzeeni kama yule nyanya wa Uganda

NA FRIDAH OKACHI

MBUNGE wa Suba Kusini Millie Mabona Odhiambo; amechangamsha wanamtandao kwa kujipa moyo kwamba huenda akajifungua siku za usoni kama ajuza wa miaka 70 nchini Uganda aliyefanikiwa kupata pacha.

Katika ukurasa wake wa Facebook, mwanasiasa huyo aliandika ujumbe wa kuwa na tumaini la kupata mtoto siku zijazo licha ya miaka yake kusonga baada ya nyanya huyo wa miaka 70 kushangaza ulimwegu kwa kujifungua watoto pacha.

Bi Odhiambo aliweka picha ya mama huyo na kuambatisha na ujumbe uliovutia mashabiki wengi kwa kumsherehekea kama mama wa mataifa mengi. Alikuwa akichangia kwenye safu ya gazeti la Daily Nation ambalo lilikuwa limechapisha taarifa hiyo.

“Kumbe, nina imani,” aliandika Bi Odhiambo.

Mashabiki walichukua fursa ya kumpa moyo kwa kumhimiza jambo hilo linaweza kufanyika licha ya kuwepo kwa utafiti wa sayansi kuwa baada ya kikomo cha hedhi “menopause” huwezi kupata ujauzito.

“Wakati wa Mungu muhimu, taarifa hii inatia moyo,” alichangia Elizabeth Sila.

Joanne Adede alimtaka kiongozi huyo kuzidi kumwamini mwenyezi Mungu kwamba anaweza kupata mtoto licha ya sayansi kupinga.

“Ndio! Ndio! Ndio! Mungu ana nguvu kuliko visingizio vyote vya kisayansi na hayo ni malimwengu,” alisema Joanne Andede.

Katika ukurasa huo, mwanahabari Elenna Gachomo-Toto Nice, ni miongoni mwa wale ambao wamejitokeza kwa kutafuta watoto na kusema aliwasamehe wote walioongea vibaya kuhusu wasio na watoto.

“Tuko wengi na imani yetu imeinuliwa. Wale wanaotucheka, watamuinamia Mwenyenzi Mungu siku za usoni,” alichangia Elenna Gachomo.

September 2023, mbunge huyo alisoma mswada wa afya ya uzazi unaohusisha wanawake kupata watoto kupitia wanawake wengine.

Katika ripoti hiyo ya mswada iliyosomwa kwa mara ya kwanza kwenye Bunge la 12, ilielezea mchango wa kupata watoto kupitia mwanamke mwingine.

Pia ripoti hiyo ilizungumzia afya ya mama.

Iwapo mswada huo utapita katika Bunge, wanawake watakaokubali kubeba ujauzito watahitaji kuwa chini ya miaka 25 na sio zaidi ya miaka 40 na wanahitaji kuzaa mtoto mmoja tu.

Soma pia: https://taifaleo.nation.co.ke/habari/kimataifa/ajuza-wa-miaka-70-akaidi-sayansi-na-kujifungua-mapacha

  • Tags

You can share this post!

Namtamani mfanyakazi wangu kimapenzi lakini amenikataa,...

Riggy G akemewa kupeleka siasa za Mungiki hafla ya heshima...

T L