• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 8:50 AM
MITAMBO: Mashini inayosaidia kupakia mazao na kuyahifadhi vyema

MITAMBO: Mashini inayosaidia kupakia mazao na kuyahifadhi vyema

NA RICHARD MAOSI

MKULIMA ambaye amejikita kwenye kilimo-biashara anaweza kukabili kero ya kupoteza mazao ya shambani kwa kutumia teknolojia sahihi ya kuhifadhi au kupakia.

“Kuna faida nyingi za kutumia teknolojia kuanzia hatua ya upanzi, usindikaji na usimamizi mzuri wa mazao wakati kwa kutoa hesabu kupitia kumbukumbu za shambani na hivyo basi matokeo yake ni kutengeneza faida,” anasema Judith Mugure kutoka eneo la Kinoo, Kaunti ya Kiambu.

Kulingana na Mugure mchakato muhimu katika sekta ya kilimo biashara, ambao umekuwa ukiwalemea wakulima wengi ni hatua ya kuhifadhi au kupakia mazao, kwani baadhi yao bado wanatumia nyenzo za kiasili kutunza lishe yao kama vile kukaushia juani.

Kwa upande mwingine, anasema kupakia na kupakua kwa njia isiyokuwa sahihi inaweza kufanya mazao kupotea kwa kuchubuka, kukauka, kupasuka , kubonyea na hata kumwagika.

Pili, anasema kuhifadhi mazao kama vile mboga katika hali ya hewa ya kawaida ni jambo gumu sana kwa sababu njia hiyo huchangia mazao mengi kuharibika.

Judy Mugure kutoka eneo la Kinoo Kaunti ya Kiambu akionesha mtambo wa nitrogen machine ambao hutumika kupakia vyakula PICHA | RICHARD MAOSI

Anasema uvmbuzi wa teknolojia ya kisasa kupitia mtambo wa nitrogen machine mkulima anaweza kupakia mazao yake, kupitia mtindo unaofahamika kama smart packaging ili chakula kiweze kudumisha ubora wa hali ya juu kwa muda mrefu.

“Hatua ya kutumia mfumo sahihi wa kupakia nafaka, mboga au matunda huwahakikishia wateja lishe salama kwa matumizi ,” anasema Mugure.

Aidha, huu ni mtambo unaotumiwa na wauzaji chakula wanaolenga masoko ya nje kama vile Uchina na Marekani, ambapo kigezo cha uzingatifu hupewa kipaumbele.

Anasema mtambo kwa jina nitrogen machine hutoa mazingira yaliyoratibiwa ili kuzuia ukuaji wa vimelea ambavyo kwa kawaida huwa ndio chanzo cha kuharibu chakula au vinywaji.

Anaeleza kuwa ni mfumo ambao huleta utunzaji wa mazingira, kwani mifuko inayotumika kuhifadhi chakula inaweza kutumika tena.

Baadhi ya mazao ambayo yanafaa kupakiwa vyema kabla ya kusafirishwa ni aina mbalimbali ya mizizi, mbegu, viazi vitamu, uyoga, maziwa asali na viazi vikuu .Kwa mfano, uyoga ni zao linaloota katika sehemu yoyote ile, msimu wa mvua nyingi na wataalam wanasema maeneo yenye mboji.

Mtaalam wa kilimo cha uyoga, Alice Wamboi kutoka kijiji cha Karuga Kaunti ya Kiambu, anasema uyoga huhifadhi kiwango kikubwa cha maji, hivyo basi huharibika haraka baada ya kuvuna.

Anasema kupitia teknolojia ya utayarishaji, usindikaji kupakia na kupakua uyoga inaweza kuwafaa wakulima wa zao hili kuhifadhi bidhaa za uyoga kwa muda mrefu

You can share this post!

NJENJE: Rwanda sasa yaipita Kenya kwenye bei bora za...

KCPE 2022: Robinson Fwaro Makokha na Otieno Lewis Omondi...

T L