• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 10:50 AM
AMINI USIAMINI: Kuna buibui wanaoweza kumla ndege

AMINI USIAMINI: Kuna buibui wanaoweza kumla ndege

NA MWORIA MUCHINA

BUIBUI wanaofahamika kama Bird-eating spiders ambao jina la kisayansi ni Theraphosa blondi huwa wakubwa sana kimaumbile.

Wana nywele kama mishale kwenye ngozi zao na hizi nywele huwa na sumu kali.

Hawa ndio buibui wakubwa duniani na wana meno marefu sana miongoni mwa buibui.

Hula viumbe kama wadudu, ndege wadogo na viumbe wengine. Wanaweza wakakaa wiki moja bila kula. Kujikinga dhidi ya maadui, buibui hawa wanaweza kurusha nywele hizo zinazofanana na mishale ambazo huwa na sumu kali.

  • Tags

You can share this post!

Uingereza yalipa familia 2 fidia ya ng’ombe 98 kwa...

Afueni kwa CHVs wa Kilifi wakianza kupokea marupurupu

T L