NA MWORIA MUCHINA
WADUDU waitwao ‘dung beetle’ au Scarabaeus satyrus kwa jina la Kisayansi, hutengeneza mipira wakitumia kinyesi cha ndovu, nyati na wanyama wengine wa porini wala nyasi.
Baadaye, wadudu hawa husukuma mipira hii wakitumia miguu yao ya nyuma hadi kwenye shimo walilochimba na hutaga mayai kwenye kinyesi hicho na kufunika mchangani. Inasemekana wadudu hao ambao hutokea nyakati za usiku, hutumia nyota na sayari za anga za juu kuwaongoza.