• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 6:07 PM
FATAKI: Wanawake walio mamlakani wasiogope kupambana na hawa wambea wanaosambaza uvumi wa uongo

FATAKI: Wanawake walio mamlakani wasiogope kupambana na hawa wambea wanaosambaza uvumi wa uongo

Na PAULINE ONGAJI

HIVI majuzi nilisoma habari ambapo mke wa rais wa Ufaransa, Bi Brigitte Macron alikuwa ameshtaki jukwaa fulani la mtandaoni kwa kueneza madai ya uwongo kuwa alizaliwa akiwa mwanamume.

Kulingana na madai hayo yaliyochapishwa kwenye tovuti ya mrengo wa kulia mwezi Septemba na kusambazwa mitandaoni, eti Bi Macron ambaye ni mama wa watoto watatu, ni mwanamke aliyebadili jinsia na kwamba alizaliwa akiwa mwanaume.

Mjadala huu uliibua hisia mseto, kejeli na matusi dhidi ya mwanamke huyu ambapo sasa umri wake na sababu kwamba amemzidi mumewe kwa miaka 25, umekuwa jukwaa la dhihaki.

Miaka michache iliyopita matusi sawa na haya yalielekezewa mke wa Rais wa zamani wa Amerika, Bi Michelle Obama, ambapo kuliibuka kikundi fulani cha watu waliotia doa mafanikio ya uongozi wa Rais Obama.

Inastaajabisha, kuhuzunisha na kuudhi kwamba hii ndio imekuwa silaha inayotumiwa kuwashambulia wanawake walio kwenye upeo wa mamlaka, na kinachoudhi hata zaidi ni kwamba vyombo vya habari vinatumika kuendeleza upuzi huu.

Mwanahabari huyo ambaye sitamtaja kwani sidhani jina lake linastaili kuwa kwenye aya moja na mwanamke wa haiba ya juu kama Bi Obama, alijitwika jukumu la kumshambulia Bi Obama kupitia shirika moja la habari nchini humo, huku akifahamu vyema kwamba kutokana na nafasi ya Bi Obama serikalini, hangemchukulia hatua ya kisheria.

Kisha tunajiuliza kwa nini wanaume wanaamini kwamba adui ya mwanamke ni mwanamke?

Wengi wanafahamu kwamba kumfananisha mwanamke na mwanamume ni dharau kuu. Pia, wengi wanajua kwamba ukimwelekezea matusi mwanamke ambaye ameafikia mengi maishani, kuna uwezekano mkubwa kwamba hatolipiza kisasi kwani akifanya hivyo, jamii itakuwa tayari kumshambulia na kutia doa sifa zake za uongozi.

Wakati umewadia kwa wanawake walio mamlakani au katika nafasi za uongozini kupambana na watu wanaowashambulia wakitumai kwamba hawatojikinga pasipo kuhukumiwa na ni matumaini yangu kwamba Bi Macron atashinda kesi hiyo na wahusika kuadhibiwa vikali.

Kuna baadhi ya watu wanaosema kwamba Bi Macron hapaswi kufuatilia wala kuwachukulia hatua za kisheria wanaoendeleza uvumi huu iwapo madai haya sio ya kweli, lakini sikubaliani na kauli hiyo.

Wakati umewadia kwa wanawake walio mamlakani au katika nafasi za uongozini kupambana na watu wanaowashambulia wakitumai kwamba hawatojikinga pasipo kuhukumiwa, na ni matumaini yangu kwamba Bi Macron atashinda kesi hiyo na wahusika kuadhibiwa vikali.

You can share this post!

Spurs wakomoa Watford na kuweka hai matumaini ya kuingia...

PENZI LA KIJANJA: Ukiweka azimio la ndoa kuwa kwenye mali,...

T L