• Nairobi
  • Last Updated May 22nd, 2024 6:07 PM
Utajuaje familia yenye mshikamano na ushirikiano mzuri?

Utajuaje familia yenye mshikamano na ushirikiano mzuri?

NA MARGARET MAINA

[email protected]

JAPO changamoto za maisha zinaweza kufanya watu kukosa utulivu, kwa baadhi ya wanafamilia, haziyumbishi mshikamano na ushirikiano wao mzuri.

Familia zenye furaha mara nyingi huwa na sifa fulani zinazofanana, na kila mwanafamilia hujitahidi kurekebisha tabia ili kuwe na mfanano fulani kuimarisha furaha.

Kula pamoja

Kula chakula cha jioni pamoja kunaweza kupunguza matukio ya matumizi mabaya ya dawa za kulevya, mimba za utotoni, na unyogovu.

Watoto wanaokula pamoja na wazazi wao wana uwezekano mkubwa wa kufanya vyema kwenye mitihani, kujithamini na hata kutumia maneno ya heshima wanapozungumza.

Ni bora zaidi mkizima runinga na kuweka kando vifaa vya kielektroniki ili mjongee mezani kula chakula cha jioni kama familia.

Kujiunganisha pamoja

Familia zenye furaha huhisi hisia kali za kuunganishwa na kila mwanafamilia. Muunganisho halisi huchukua kama dakika tano kwa siku. Utawaona wanafamilia wakiwa pamoja wakati wa kazi ya nyumbani. Kwa mfano utaona mama na mtoto wakipika pamoja au ndugu wakisoma vitabu kabla ya kulala, na kadhalika.

Kuwa na ratiba nzuri na tulivu asubuhi na yenye furaha zaidi kwa kujiandaa usiku uliotangulia au kuamka mapema zaidi.

Jane, mama wa wavulana wawili, wenye umri wa miaka 4 na 2, anasema kwamba dakika 30 za kwanza asubuhi na dakika 30 za mwisho kabla ya kulala husaidia familia yake kuwa na utulivu na kuhisi kupendwa.

Tafuta utimilifu

Japo vifaa vya kisasa vya kielektroniki au ala za muziki huleta furaha ya muda mfupi, ni muhimu kutafuta uhalisia. Huu uhalisia utapatikana kwa kukaa na watoto na kuwapigia stori ili nao waone furaha inatoka kwa familia yenyewe.

Mazoea ya kutafuta furaha mtandaoni yanaleta hamu na matarajio yanayozidi hali halisia. Hapa ndipo tunapata aibu kubwa. Mtu anakosa furaha kwa sababu ana matarajio yasiyo ya kweli au yasiyoweza kutimizwa katika mazingira ya sasa.

Watoto wanaohimizwa mapema kushiriki katika shughuli wanazofurahia na zinazokuza nguvu zao hukua na kuwa watu wazima wenye furaha.

Unda jumuiya

Shirikia shughuli za maendeleo na ustawi katika mtaa wako, kanisani, au kwenye shule ya mtoto wako.

“Watoto wangu huenda kwenye mbuga ya wanyama na kutembelea shangazi yao,” Jane anasema.

Anaongeza: “Wanapoenda huko, mimi na mume wangu hupata wakati mzuri wa kutulia nyumbani au kuenda kutembea.”

Kubali hisia

Mwelewe mtoto wako anapokasirika, sikiliza na uthibitishe hisia zake. Epuka kuchukua tabia ya mtoto wako binafsi au kuharakisha kurekebisha matatizo yake. Wakipewa fursa, mara nyingi watoto wanaweza kutatua matatizo na changamoto zinazowakabili kwa amani na kujadiliana na ndugu na dada bila kuingiliwa na wazazi.

  • Tags

You can share this post!

Wabunge wa Azimio waliokwepa kura au kuunga mkono Mswada wa...

Serikali ya Kenya Kwanza yapunguza pesa za wazee

T L