• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 6:07 PM
BENSON MATHEKA: Kenya Kwanza haifai kusuta Azimio kwenda kortini kupinga matokeo ya urais

BENSON MATHEKA: Kenya Kwanza haifai kusuta Azimio kwenda kortini kupinga matokeo ya urais

NA BENSON MATHEKA

MUUNGANO wa Azimio la Umoja One Kenya umewasilisha kesi katika Mahakama ya Juu kupinga matokeo ya kura ya urais kwenye uchaguzi mkuu uliopita huku ule wa Kenya Kwanza na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ikipanga kujitetea.

Hatua ya Azimio inaonyesha wanaheshimu utawala wa Katiba na Sheria. Katika kesi hiyo watawasilisha ushahidi wao mbele ya majaji wa Mahakama ya Juu ambao watasikiliza kesi.

Upande wa Kenya Kwanza na IEBC, akiwemo mwenyekiti wake Wafula Chebukati watajitetea kabla ya majaji kutoa uamuzi wao.

Kwa kuwa kila upande umekuwa ukihimiza mwingine kwenda kortini usiporidhika na matokeo, kuna haja ya kuheshimu uamuzi wa Azimio wa kuwasilisha kesi kortini.

Inasikitisha kuona baadhi ya wanachama wa Kenya Kwanza wakitoa matamshi yanaoyoashiria kusuta Azimio kwa kwenda kortini.

Japo wako na haki ya kutoa maoni yao, wanafaa kuheshimu haki ya Azimio ya kutafuta haki kortini.

Kinaya ni kwamba kabla ya uchaguzi, wanaosuta Azimio kwa kuwasilisha kesi, walikuwa wameahidi kwenda kortini iwapo hawangeridhishwa na matokeo ya uchaguzi.

Swali ni je, nini kimebadilika sasa waweze kusuta wapinzani wao kwa haki yao ya kwenda kortini?

Maoni ya wanasiasa hao yanaonyesha kuwa hawathamini au hawamaanishi wanachosema bali huwa wanakisema kufurahisha wafuasi wao wakati fulani na kubadilika jinsi mazingira yanavyobadilika. Hii pia ni haki yao.

Katiba inampa kila Mkenya uhuru wa kwenda mahakamani kutafuta haki na anayesuta au kuzuia yeyote kutafuta haki kortini ni adui wa utawala wa katiba na sheria.

Haki ya mtu haifai kuzuia au kukandamiza haki ya mtu mwingine. Utawala wa kikatiba na sheria unafaa kufurahiwa na kila Mkenya.

  • Tags

You can share this post!

Kivutha Kibwana kushirikiana na Kenya Kwanza

CHARLES WASONGA: Wabunge watekeleze wajibu wao bila...

T L