• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 6:07 PM
JUMA NAMLOLA: Krismasi iwe mwalimu kuhusu kuwajali wengine na kuunganisha ukoo

JUMA NAMLOLA: Krismasi iwe mwalimu kuhusu kuwajali wengine na kuunganisha ukoo

KESHO ni ile siku ambayo mamilioni ya waumini wa dini ya Ukristo wanasherehekea ulimwengu mzima.

Kwa niaba yangu na usimamizi mzima wa gazeti hili, nchukua fursa hii kuwatakia Heri Njema ya siku hiyo.Kama kawaida ya siku za kuadhimishwa kiroho, hii ni nafasi bora kwa walio nacho kuwajali mayatima, kuwatembelea wagonjwa na kuwafariki waliopatwa na misiba ya aina mbalimbali.

Kuna wale waliotembelea wazazi wao mashambani. Kwa mipango ya Mungu, huu ndio msimu ambapo hata wale wana wapotevu, hukumbuka kwamba walizaliwa.Kwa watakaofanikiwa kuwatembelea wazazi au jamaa zao vijijini, mnastahili pongezi.

Sisi tuliokwama mijini kutokana na shughuli za kazi, mtuombee wakati mwingine tupate nafasi, nguvu na uwezo wa kutembelea tulikotoka.Ingawa watu wengine hudhani kesho ni siku ya kusherehekea pekee, Krismasi ni muda ambapo watu hutakiwa kupata mafunzo muhimu ya maisha.

La kwanza ni kuwa, kila mtu ana pahali anapopaita kwao. Hili lisitumiwe kikabila kuwatenganisha watu au kuwafukuza kutoka eneo moja la nchi. Katiba yetu inatoa hakikisho kuwa kila mtu anaweza kuishi na kuendesha shughuli zake popote Kenya.

Mtu kuwa na kwao yafaa itumike kuwahimiza watu wawe na makao mazuri wanakotoka. Ni aibu kwa mtu kuishi kwenye nyumba iliyo na vyombo vya kifahari, lakini akifika kwao mashambani na familia yake, aanze kutafuta pahali pa kulala.Pili, kuunganisha ukoo.

Kuwapeleka watu wa familia yako na kuwaonyesha mke na watoto watu wa kwenu ni muhimu. Mwanadamu huishi kwa kutegemea wengine. Ni muhimu kujulisha watu wake kwao ili wajuane.Lakini hata kama Krismasi na Mwaka Mpya ni muda wa watu kusherehekea, itakuwa vyema watu wasiwasahau wasio na uwezo.

You can share this post!

Rais wa zamani Tunisia asukumwa jela miaka 4

Wafuasi wa Azimio wasema mambo bado

T L