• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 1:05 PM
Arsenal wakomoa Villa na kukalia vizuri katika nafasi ya nne EPL

Arsenal wakomoa Villa na kukalia vizuri katika nafasi ya nne EPL

Na MASHIRIKA

KOCHA Mikel Arteta wa Arsenal alikuwa mwingi wa sifa kwa kikosi chake kilichokomoa Aston Villa 1-0 mnamo Jumamosi usiku katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) na kuimarisha nafasi ya kukamilisha kampeni za msimu huu ndani ya mduara wa nne-bora.

Bao la pekee katika mchuano huo lilipachikwa wavuni na Bukayo Saka. Ushindi wa Arsenal ulikuwa wao wa sita kutokana na mechi saba zilizopita na sasa wanakamata nafasi ya nne kwa alama 54, tano nyuma ya Chelsea wanaoshikilia nafasi ya tatu.

Ni pengo la alama nne kwa sasa ndilo linatamalaki kati ya Arsenal na nambari tano Manchester United ambao wametandaza mchuano mmoja zaidi kuliko mechi 28 ambazo zimesakatwa na Arsenal.

“Kikosi kinazidi kuimarika. Wachezaji wanacheza kwa kuonana. Kuwa miongoni mwa vikosi bora kunalazimu timu kushinda mechi za nyumbani na ugenini. Huo ndio mtindo tunaotaka kuendeleza ili kuweka hai matumaini ya kumaliza msimu ndani ya orodha ya nne-bora,” akasema Arteta.

Arsenal wanawania fursa ya kushiriki soka ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) kwa mara ya kwanza baada ya kipindi cha miaka mitano iliyopita. Bao la Saka aliyemhangaisha sana beki Ashley Young, 36, aliyewajibishwa katika nafasi ya Lucas Digne, lilikuwa lake la 10 katika mashindano yote kufikia sasa msimu huu.

Chini ya kocha Steven Gerrard, Villa walijitosa ugani wakiwa na kiu ya kujinyanyua baada ya kupoteza mechi tisa kati ya 11 iliyopita dhidi ya vikosi vinavyoshikilia nafasi nane za kwanza kwenye msimamo wa jedwali la EPL.

Kikosi hicho kwa sasa kinashikilia nafasi ya tisa kwa alama 36 japo pengo la pointi 10 linatamalaki kati yao na Wolves wanaofunga mduara wa nane-bora.

You can share this post!

Rais kukutana na wanabodaboda

Chelsea wapewa Real Madrid katika robo-fainali ya UEFA

T L