• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 1:05 PM
Brighton yazamisha Spurs

Brighton yazamisha Spurs

Na MASHIRIKA

BAO kutoka kwa Leandro Trossard mwishoni mwa kipindi cha pili liliwezesha Brighton kusajili ushindi wa 1-0 dhidi ya Tottenham Hotspur na kuyumbisha matumaini ya masogora hao wa kocha Antonio Conte kumaliza kampeni za Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) msimu huu ndani ya mduara wa nne-bora.

Steven Bergwijn alipoteza nafasi murua ya kusawazishia Spurs sekunde chache kabla ya kipenga cha kuashiria mwisho wa mchezo kupulizwa.

Matokeo hayo yalisaza Spurs katika nafasi ya nne jedwalini kwa alama 57, tatu zaidi kuliko Manchester United na Arsenal. Brighton kwa sasa wanakamata nafasi ya 10 jedwalini kwa alama 40 sawa na Leicester City.

Spurs watavaana na Liverpool mnamo Mei 7 kabla ya kumenyana na Arsenal siku tano baadaye katika mechi zinazotarajiwa kuamua kikosi kitakachoungana na Chelsea, Liverpool na Manchester City ndani ya mduara wa nne-bora na kufuzu kwa soka ya UEFA msimu ujao wa 2022-23.

Ushindi wa Brighton ulikuwa wao wa pili mfululizo jijini London baada ya kutandika Arsenal 2-1 katika mechi ya awali ligini. Kikosi hicho cha kocha Graham Potter sasa kimejivunia pointi 25 kati ya 40 wanazojivunia kutokana na mechi za ugenini.

Licha ya kusalia na mechi dhidi ya Man-United na West Ham msimu huu, Brighton wanapigiwa upatu wa kufuzu kwa soka ya bara Ulaya muhula ujao na kumaliza kampeni za EPL katika nafasi bora zaidi katika historia.

MATOKEO YA EPL (Jumamosi):

Tottenham 0-1 Brighton

Man-United 3-2 Norwich

Southampton 1-0 Arsenal

Watford 1-2 Brentford

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Walioanguka mchujo UDA kutozwa hadi Sh200,000

Southampton yaendeleza masaibu ya Arsenal

T L