• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 10:27 AM
Chelsea waomba kucheza na Middlesbrough bila mashabiki katika robo-fainali ya Kombe la FA

Chelsea waomba kucheza na Middlesbrough bila mashabiki katika robo-fainali ya Kombe la FA

Na MASHIRIKA

CHELSEA wameomba mechi ya robo-fainali ya Kombe la FA kati yao na Middlesbrough mnamo Machi 19, 2022 kuchezwa bila mashabiki uwanjani “kwa ajili ya kudumisha uadilifu kimichezo”.

Serikali ilitoa leseni maalumu kuruhusu Chelsea kuendelea kucheza baada ya kufungia mali ya mmiliki wao Roman Abramovich ambaye ni bwanyenye raia wa Urusi.

Chini ya masharti ya leseni, klabu ya Chelsea haiwezi kuuza tiketi za mechi. Hatua hiyo ilianzishwa ili kumzuia Abramovich, ambaye anatazamia kuiuza klabu hiyo kutopata faida.

Abramovic amepigwa marufuku kuwa mkurugenzi wa klabu na mchakato wa uuzaji wa Chelsea umecheleweshwa baada ya serikali ya Uingereza kumwekea bwanyenye huyo vikwazo kutokana na uhusiano wake wa karibu na rais wa Urusi, Vladimir Putin.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Baadhi ya wakazi wa Thika wafanya maandamano wakitaka Ruto...

Mshukiwa mkuu wa bodaboda aliyedhulumu mwanamke anyakwa

T L