• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 12:35 PM
Dereva Kimathi atarajia Croatia Rally

Dereva Kimathi atarajia Croatia Rally

Na GEOFFREY ANENE

BINGWA wa Afrika kitengo cha chipukizi cha mbio za magari 2021 McRae Kimathi na mwelekezi wake Mwangi Kioni wanatarajia duru ya dunia ya Croatia kuwa ngumu hapo Aprili 21-24.

Akizungumza baada ya kuwasili katika taifa hilo la bara Ulaya, walisema kupaisha gari la mashindano kwenye lami kwa mara ya kwanza kutakuwa na changomoto zake.

“Ni mara ya kwanza nitashindana kwenye lami. Habari ambazo nimepata ni kuwa ina changomoto zake, ni ya kasi sana. Hata hivyo, tutachukua mambo yatakavyokuja ili tupate pointi,” alinukuliwa na vyombo vya habari akisema nchini Croatia, Jumamosi.

Aliongeza, “Uswidi ilikuwa baridi na ninatumai hapa Croatia hali ya anga itakuwa nzuri ili tufurahie barabara na pia hali ya anga.”

Kimathi,27, alifanya duru yake ya kwanza kabisa ya Mbio za Magari Duniani (WRC) mnamo Februari 24-27, akimaliza nambari nne katika kitengo cha chipukizi kwenye theluji.

Runinga ya NTV ilipata haki za kupeperusha duru za Mbio za Magari Duniani (WRC) nchini Kenya kwa hivyo mashabiki kutoka Kenya watapata burudani ya Croatia Rally kupitia runinga hiyo ya kampuni ya Nation Media Group na pia tovuti ya WRC.

Kimathi anayeendesha gari la Ford Fiesta R3 yuko katika mradi wa madereva chipukizi kukuzwa na Shirikisho la Mbio za Magari Duniani (FIA) maarufu kama FIA Rally Star. Ana alama 12 kutokana na duru ya Uswidi.

  • Tags

You can share this post!

Trailblazers yapania kutinga fainali za Klabu Bingwa Afrika...

Ronaldo abeba Man-United dhidi ya Norwich City

T L