• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 9:48 PM
Dortmund wacharaza RB Leipzig na kutia kapuni taji la German Cup

Dortmund wacharaza RB Leipzig na kutia kapuni taji la German Cup

Na MASHIRIKA

JADON Sancho na Erling Braut Haaland walifunga mabao mawili kila mmoja na kusaidia Borussia Dortmund kutia kibindoni taji la German Cup baada ya kuwapepeta RB Leipzig 4-1 mnamo Alhamisi usiku.

Sancho, 21, aliyefungulia waajiri wake karamu ya  mabao kabla ya kupachika wavuni goli la tatu kabla ya mwisho wa kipindi cha kwanza, ndiye mchezaji mchanga zaidi kuwahi kufunga mabao mawili katika fainali ya German Cup.

Haaland alipachika wavuni goli la pili la Dortmund katika dakika ya 28 kabla ya kufunga la pili mwishoni mwa kipindi cha pili baada ya Dani Olmo kuwafutia Leipzig machozi katika dakika ya 71.

Dortmund kwa sasa wametia kapuni ufalme wa German Cup mara tano katika historia.

Kocha Julian Nagelsmann wa Leipzig ambaye atadhibiti mikoba ya Bayern Munich msimu ujao, alikuwa na matarajio makubwa ya kukamilisha kipindi cha kuhudumu kwake kambini mwa kikosi hicho kwa kujizolea taji lake la kwanza katika ulingo wa ukufunzi.

Hata hivyo, ni Edin Terzic aliye na umri wa miaka 38 ndiye aliweka historia ya kuwa kocha mchanga zaidi kunyanyua taji la DFB-Pokal baada ya Thomas Schaaf (miaka 38 na siku 43) mnamo 1998-99 akidhibiti mikoba ya Werder Bremen.

Baada ya kufuma wavuni mabao mawili dhidi ya Leipzig, Haaland kwa sasa anajivunia magoli 39 kutokana na 39 ambazo amechezea Dortmund kufikia sasa msimu huu.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Mogotio United yazidi kung’aa

Real Madrid yapepeta Granada na kuendeleza presha kwa...