• Nairobi
  • Last Updated June 12th, 2024 4:24 PM
Karan Patel ndiye mfalme wa Eldoret Rally

Karan Patel ndiye mfalme wa Eldoret Rally

Na GEOFFREY ANENE

DEREVA Karan Patel amezoa ushindi wake wa nne mfululizo kwenye Mbio za Magari za Kitaifa Kenya (KNRC) mwaka 2022 baada ya kutawala duru ya Eldoret Rally katika milima ya Cherangany, Jumamosi.

Karan, ambaye alifungua msimu kwa kubeba taji la Kajiado Rally mwezi Januari kabla ya kuongeza ubingwa wa Nakuru Rally mwezi Machi na duru ya Afrika ya Equator Rally mwezi Aprili, alishinda Eldoret Rally baada ya kuchukua uongozi kutoka kwa Jasmeet Chana katika kilomita 34.48 za mwisho.

Alikamilisha dakika moja na sekunde 15 mbele ya Jasmeet, wote wakipaisha Mitsubishi Evo X.

Matokeo (saba-bora)

1.Karan Patel/Tauseef Khan (EVOX) saa 02:06.13.5

2. Jasmeet Chana/Ravi Chana (EVOX) 02:07.00.7

3. Ghalib Hajee/Riyaz Ismail (EVOX) 02:16.02.8

4. Kush Patel/Mudasar Chaudry (Subaru) 02:16.38.3

5. Sam Karangatha/Steven Nyorri (Datsun 180B) 2:35.30.4

6. Leonardo Varese/KIgondu Kareithi (Toyota Auris) 2:42.54.8

7. Gideon Kimani/LInet Ayuko (Subaru) 2:54.15. 5

  • Tags

You can share this post!

Weta sasa kuvumisha Ruto kikamilifu akisubiri kutetea kiti...

Ugatuzi: Kilio cha magavana

T L