• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 6:07 PM
Man-City na Newcastle nguvu sawa katika EPL ugani St James’ Park

Man-City na Newcastle nguvu sawa katika EPL ugani St James’ Park

Na MASHIRIKA

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), Manchester City, walitoka nyuma kwa mabao 3-1 na kulazimishia wenyeji wao Newcastle United sare ya 3-3 katika kipute hicho mnamo Jumapili ugani St James’ Park.

Newcastle wanaonolewa na kocha Eddie Howe walikuwa wakijivunia uongozi wa mabao mawili kufikia dakika ya 54 kabla ya Erling Haaland na Bernardo Silva kusawazisha mambo chini ya dakika nne za kipindi cha pili na kudumisha rekodi ya kutoshindwa kwa Man-City ligini msimu huu.

Man-City walifungua ukurasa wa mabao kupitia kwa Ilkay Gundogan baada ya kumwacha hoi kipa Nick Pope katika dakika ya tano. Hata hivyo, Newcastle walisawazisha kupitia kwa Miguel Almiron baada ya kushirikiana vilivyo na fowadi Allan Saint-Maximin.

Mabao mengine ya Newcastle yalijazwa kimiani na Callum Wilson na Kieran Trippier aliyeagana na Man-City mnamo 2012.

Man-City walioanza wikendi wakiongoza jedwali la EPL, walihitaji ushindi wa angalau mabao mawili kwa nunge dhidi ya Newcastle ili kudengua Arsenal kileleni.

Bao la Gundogan lilikuwa la kwanza kwa Newcastle kufungwa katika EPL msimu huu baada ya kufungua kampeni zao kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya limbukeni Nottingham Forest kisha kuambulia sare tasa dhidi ya Brighton.

Kichapo kwa Man-City kingalikuwa chao cha kwanza kupokea katika EPL ugenini tangu Agosti 15, 2021 walipotandikwa 1-0 na Tottenham Hotspur.

Man-City kwa sasa wanashikilia nafasi ya pili kwenye jedwali la EPL kwa alama saba, mbili zaidi kuliko nambari sita Newcastle.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

MWALIMU WA WIKI: Mwalimu mbobevu na mtunzi chipukizi

Real Madrid wadengua vipusa wa Man-City kwenye gozi la UEFA

T L