• Nairobi
  • Last Updated February 25th, 2024 11:30 AM
Mark Zuckerberg auguza jeraha la goti akijiandaa kushiriki shindano la karate

Mark Zuckerberg auguza jeraha la goti akijiandaa kushiriki shindano la karate

NA FRIDAH OKACHI

MWANZILISHI wa Facebook mtandao wa kijamii ambao kwa sasa unafahamika Meta, Mark Zuckerberg alifanyiwa upasuaji wa goti baada ya kupata jeraha baya wakati wa mazoezi.

Bw Zuckerberg alipata jeraha hilo wakati wa mazoezi ya karate, ambapo anajiandaa kwa mashindano yanayotarajiwa kufanyika ya sanaa ya kijeshi.

Kupitia chapisho Instagram na Facebook mnamo Novemba 3, 2023, alisema wakati wa mazoezi hayo alianza kuhisi uchungu kwenye mishipa.

“Asante kwa madaktari na kikosi kinachonihudumia. Nipo katika harakati za kupona. Nilikuwa nikifanya mazoezi kwa ajili ya Pambano la Karate (MMA) mapema 2024, lakini sasa hilo limechelewa kidogo. Bado nalisubiria kwa hamu baada ya kupona. Asante kwa kila mtu kwa upendo mlioonyesha na msaada,” Bw Zuckerberg aliandika.

Mjasirimali huyo wa kimitandao ni raibu wa karate.

Wakati mwingi huchapisha na kuonyeshana video na picha akishiriki mazoezi ya mchezo huo.

Licha ya kulazwa hospitalini, bosi huyo wa Meta mwenye umri wa miaka 39 alisema ataendelea kufanya mazoezi kwa ajili ya mashindano ya karate (MMA) mapema 2024.

Mark Zuckerberg ni mmoja wa wabunifu wa kumbi za kiteknolojia, ambazo zimeleta mabadiliko makuu duniani, ikiwa ni pamoja na kurahisha watu kujuana na kuonana na hata kuendeleza biashara.

Mitandao ya Facebook, Instagram, Whatsapp na Threads anazidi kuiboresha kutokana na tajriba ya teknolojia aliyo nayo.

 

 

  • Tags

You can share this post!

Kalonzo ampongeza Mdhibiti wa Bajeti kwa kufichua serikali...

Tuache kurushiana lawama tunapopigana na Al-Shabaab, Duale...

T L