• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 6:50 AM
Mbappe ndiye mwanasoka mwenye thamani kubwa zaidi duniani

Mbappe ndiye mwanasoka mwenye thamani kubwa zaidi duniani

Na MASHIRIKA

KYLIAN Mbappe, Vinicius Jr na Erling Haaland ndio wachezaji wenye thamani ya juu zaidi duniani. Haya ni kwa mujibu wa shirika la CIES Football Observatory.

Mbappe, 23, aliyekataa ofa ya kujiunga na Real Madrid na badala yake kurefusha muda wa kuhudumu kwake kambini mwa Paris Saint-Germain (PSG), anaongoza orodha hiyo kwa kima cha pauni 175.7m.

Fowadi wa Real na timu ya taifa ya Brazil, Vinicius Jr, anakamata nafasi ya pili kwa pauni 158.3m huku Haaland wa Manchester City na Norway akiwa wa tatu kwa pauni 130.4m.

Kiungo chipukizi wa Borussia Dortmund, Jude Bellingham (pauni 114.1m) ndiye sogora mwenye thamani ya juu zaidi kutoka Uingereza. Anashikilia nafasi ya tano kwenye orodha, mbele ya mchezaji mwenzake kambini mwa Uingeeza, Phil Foden wa Man-City anayeshikilia nafasi ya sita (pauni 105.9m).

Klabu za Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) zinatamalaki orodha hiyo kwa wachezaji 41 kutokana na wachezaji 100.

Baada ya kukataa kuhamia Real walioshinda taji la Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) mnamo 2021-22, Mbappe alitia saini mkataba mpya wa miaka mitatu kambini mwa PSG. Mshindi huyo wa Kombe la Dunia 2018, alipachika wavuni mabao 28 katika Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) mnamo 2021-22 na kuongoza PSG kunyanyua taji la kivumbi hicho.

Haaland, 21, anatarajiwa kuwa tegemeo kubwa la Man-City mnamo 2022-23 baada ya kuagana na Dortmund kwa kima cha pauni 51.2m.

Mchezaji Bora wa EPL mnamo 2021-22, Kevin de Bruyne wa Man-City mwenye umri wa miaka 30, ndiye mchezaji mkongwe zaidi katika orodha hiyo ya 100-bora. Thamani yake ni pauni 48.9m huku Gavi wa Barcelona (pauni 49.9) akiwa sogora mchanga zaidi.

Gianluigi Donnarumma wa PSG aliyesaidia Italia kunyanyua taji la Euro 2020, ndiye kipa mwenye thamani kubwa zaidi. Anashikilia nafasi ya 41 kwa pauni 62.9m.

Liverpool walioambulia nafasi za pili kwenye EPL na UEFA msimu huu wanawakilishwa na sajili mpya Luis Diaz (pauni 94) aliyetua ugani Anfield mnamo Januari 2022.

Wanasoka watatu wa Barcelona – Pedri, Ferran Torres na Frenkie de Jong anayehusishwa pakubwa na Manchester United, pia wametiwa ndani ya orodha ya 10-bora.

Wanasoka wa Uingereza – Jadon Sancho (pauni 88.1m), Mason Mount (pauni 85.7m) na Bukayo Saka (pauni 85.6m) wanakamata nafasi za 13, 14, na 15 mtawalia.

Darwin Nunez (pauni 59.9), anayemezewa sana na Benfica ya Ureno ndiye mwanasoka mwenye thamani ya juu kabisa miongoni mwa masogora wanaotandaza soka nje ya ligi kuu tano za bara Ulaya.

WANASOKA 10-BORA WENYE THAMANI KUBWA ZAIDI DUNIANI:

Mchezaji Klabu Thamani
Kylian Mbappe
Paris St-Germain £175.7m

 

Vinicius Jr Real Madrid

 

£158.3m
Erling Haaland Borussia Dortmund £130.4m
Pedri Barcelona

 

£115.4m
Jude Bellingham Borussia Dortmund £114.2m
Phil Foden Manchester City £105.9m

 

Frenkie de Jong Barcelona £96.1m
Luis Diaz Liverpool £94.0m
Ruben Dias Manchester City £93.6m
Ferran Torres Barcelona £93.5m

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Kang’ata apuuza madai kuhusu kuzimwa kwake

Messi aweka rekodi ya ufungaji mabao kimataifa

T L