• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 10:50 AM
Msimu wa 2022-23 Ligi ya Divisheni ya Kwanza wanawake kufika kilele wikendi

Msimu wa 2022-23 Ligi ya Divisheni ya Kwanza wanawake kufika kilele wikendi

NA TOTO AREGE 

IMESALIA awamu moja tu ya mechi za Ligi Kuu ya Wanawake ya Divisheni ya Kwanza (KWPLDV1L) msimu wa 2022/23, kufikia kikomo rasmi.

Jumla ya timu 15 zitashushwa daraja. Timu 31 zilishiriki katika ligi hiyo ambapo, zimegawanywa kwenye zoni A na B ambayo ina timu 15 na 16 mtawalia.

Ushindani mkali unashuhudiwa kwenye Zoni B, ambapo Bungoma Queens (48), Gideon’s Starlets (46), Kisped Queens (45) na Soccer Assassins (43) ambao wameshikilia nafasi ya kwanza, pili, tatu na nne mtawalia wanatofautiana na alama chache.

Kati ya timu hizo nne, haijulikani ni timu gani itajiunga na Ligi Kuu ya Wanawake nchini (KWPL) msimu ujao hadi mechi ya mwisho itakapo chezwa.

Katika Zoni B, hali ni kama hiyo hiyo. Hata baada ya kutangazwa kujiunga na KWPL wiki mbili zilizo pita, Kibra Women Soccer wanaongoza kwenye jedwali na alama 56.

Nafasi ya pili Uweza Women (49), Mathare United Women (46) na Mombasa Olympic (43) wanafunga nne bora kwenye msimamo wa ligi.

Moja kati ya timu hizi tatu ambayo itamaliza nafasi ya pili, itacheza na timu ya nafasi ya pili ya Zoni A katika mechi ya mchujo. Mshindi wa mechi hiyo moja kwa moja atapanda daraja na kujiunga na KWPL.

Raundi ya 22 imepangwa kuchezwa wikendi hii. Wakati uo huo, ushindani mkali wa kuwania Kiatu cha dhahabu.

Mshambulizi wa Mombasa Olympic ya Kundi A ndiye mfungaji bora wa jumla na mabao 28. Valary Nekesa wa Soccer Assassins ya Zoni B ni wa pili na mabao 25.

Winnie Gwatenda kutoka Kibra Soccer Ladies anafuata nafasi ya pili na mabao 23. Calta Wanjala wa Falling Waters Barcelona anafunga nne bora na mabao 14.

Washindi wa Zoni A na B wataenda nyumbani na Sh500,000 kila mmoja.

Mechi ya mshindi wa jumla wa ligi itachezwa Agosti 6, 2023 mjini Nakuru. Mshindi ataenda nyumbani na kikombe.

  • Tags

You can share this post!

KRU yashusha bei ya tiketi kutoka Sh300 hadi Sh100 kujaza...

Maseneta waelezwa sababu ya neti hafifu kuingizwa nchini

T L