• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 10:55 AM
Mwendwa anaswa tena

Mwendwa anaswa tena

Na RICHARD MUNGUTI

RAIS wa shirikisho la kandanda nchini (FKF) Nick Mwendwa alikamatwa tena jana siku moja baada ya kuachiliwa na mahakama.

Bw Mwendwa alikamatwa na kurushwa ndani ya gari ambalo halikuwa na nambari za usajili kisha akapelekwa moja kwa moja hadi makao makuu ya idara ya uchunguzi wa jinai (DCI).Gari la kinara huyo wa FKF ilizuiliwa na magari mawili kisha maafisa wa polisi wakamtoa katika gari lake na kumrusha ndani ya gari lao.

Kufuatia tukio hilo wakili Eric Mutua aliwaandikia barua Inspekta Jenerali wa Polisi (IG) na Mkurugenzi wa Idara ya Uchunguzi wa Jinai(DCI) George Kinoti akilalamikia matumizi mabaya ya mamlaka ya polisi.Bw Mutua aliwataka IG na DCI wamwachilie Mwendwa kwa dhamana na kumweleza siku ile atakapofika mahakamani.

Awali Mwendwa alishikwa Novemba 12 kwa madai ya ubadhirifu wa Sh513 lakini mahakamani wakasema ni Sh38 miliioni..Mwendwa alitiwa nguvuni akitoka katika makazi yake mtaani Runda Nairobi. Alikuwa anaelekea kati kati mwa jiji.

Katika barua hiyo kwa IG na DCI Bw Mutua alisema kukamatwa kwa Mwendwa ni mbinu ya kumnyamazisha asiendelee na kesi ambayo Serikali imeshtakiwa na FKF kutimua kamati ya kusimamia kandanda chini ya uenyekiti wa Jaji (mstaafu) Aaron Ringera.

Kamati hiyo iliteuliwa na Waziri wa Michezo Amina Mohamed kusimamia masuala ya kambumbu.Bw Mutua ameomba Mwendwa aachiliwe kwa dhamana.“Endapo Mwendwa hataachiliwa kwa dhamana basi kesi itawasilishwa dhidi ya IG na DCI pamoja na maafisa wa polisi waliomtia nguvuni kumlipa fidia kwa kukaidi haki zake,” Mutua amesema katika barua hiyo.

Pia amesema atamlalamkia Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) na mamlaka huru ya polisi (IPOA) tabia ya polisi waliomkamata Mwendwa hata baada ya kuchiliwa huru na mahakama na kurudishiwa dhamana aliyokuwa amelipa ya Sh4milioni.

You can share this post!

Timu 10 kushiri Mini-ligi ya Kaunti ya Taita Taveta wikendi

Mabwanyenye wapya Newcastle nao pia wajishasha kuwania...

T L