• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 10:50 AM
Namwamba ahofia mabadiliko ya tabianchi yatavuruga michezo

Namwamba ahofia mabadiliko ya tabianchi yatavuruga michezo

NA AYUMBA AYODI

KENYA inahofia mambo yanaweza kuharibika zaidi katika sekta ya michezo ikiwa hatua madhubuti hazitachukuliwa kudhibiti mabadiliko ya tabianchi ambayo tayari yameathiri maisha ya wanamichezo.

Waziri wa Michezo Ababu Namwamba na rais wa Shirikisho la Riadha Kenya (AK) Jack Tuwei wanataka ulimwengu uchukulie kwa uzito suala hilo wakisema kuwa sehemu kadha duniani zitashindwa kuandaa mashindano hivi karibuni kwa sababu ya harufu ama joto linalopanda.

Katika hotuba yake mjini Sharm El-Sheikh nchini Misri wakati wa kongamano la Umoja wa Mataifa kuhusu kazi inayofanywa na serikali, sekta ya kibinafsi na asasi za kiraia kuhusu tabia ya nchi, Namwamba alisema wakati umewadia wa kuimarisha hatua badala ya kutoa maneno ya kujitolea.

“Ulimwengu unafaa kuharakisha kutoka kutoa maneno na ufanye kazi. Wakati wa kushughulikia suala hili ni sasa!” alisema Namwamba.

Bila ya hatua muhimu kuchukuliwa kuhusu tabia ya nchi, Tuwei, ambaye pia yuko Sharm El-Sheikh, alisema kuwa ulimwengu uko katika hatari ya kupoteza sehemu za kuandaa mashindano kwa sababu ya joto linaloendelea kupanda.

Namwamba alisema kuwa AK iko mstari wa mbele katika ulimwengu wa michezo baada ya kuahidi kupunguza kwa asilimia 50 ya utokezaji wa joto kufikia mwaka 2030 na kufika sifuri mwaka 2040.

Namwamba alieleza kujivunia kuwa AK ndio ya kwanza kutoka wanachama 214 wa Shirikisho la Riadha Duniani kusaini na kuunga mkono mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kupitia michezo chini ya Umoja wa Mataifa (UNFCCC).

TAFSIRI: GEOFFREY ANENE

  • Tags

You can share this post!

Pendekezo mifumo ya kilimo itathminiwe kusaidia kuangazia...

Ruto, Raila wang’ang’ania IEBC

T L