• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
Ndume 3 ulingoni kwa ndondi za Serbia

Ndume 3 ulingoni kwa ndondi za Serbia

Na CHARLES ONGADI

MABONDIA watatu wa timu ya taifa ‘Hit Squad’ watapanda ulingoni leo katika juhudi za kusaka medali katika mashindano yanayoendelea ya Dunia katika ukumbi wa Stark Arena, Belgrade nchini Serbia.

Nahodha Nick ‘Commander’ Okoth atakabiliana na Alexy De La Cruise kutoka Jamhuri ya Kidrmokrasia ya Dominica katika pigano la uzito wa light. Naye Boniface Mogunde Maina atadundana na Begiri Alba wa Albania katika uzito wa light Middle.

Mogunde anashiriki kwa mara ya kwànza katika uzito huu baada ya kuwakilisha taifa kwa kipindi kirefu katika uzito wa welter ambayo kwa sasa inashikiliwa na Joseph ‘Shigz’ Shigali.

Bondia mwengine anayetarajiwa kupeperusha bendera ya taifa ni Hezron Maghanga Sabat atakayepigana na Alhandawi Riyad wa Jordan katika uzito mpya katika Mashindano haya wa Cruise.

Mara ya mwisho Kenya kushinda medali katika mashindano haya ni mwaka wa 1978 kupitia Steve ‘ Desty’ Muchoki aliyemcharaza Jorge Hernandez wa Cuba katika uzito wa light fly na kunyanyua.medali ya dhahabu

You can share this post!

Shahbal atetea mradi wa nyumba Buxton

Kenya yakusudia kuchanja raia 5m kufikia Desemba

T L