• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 6:36 PM
Rangers kumenyana na Dortmund kwenye mchujo wa Europa League

Rangers kumenyana na Dortmund kwenye mchujo wa Europa League

Na MASHIRIKA

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Scotland, Rangers, watapimana ubabe na Borussia Dortmund ya Ujerumani katika mchujo wa raundi ya muondoano kwenye Europa League msimu huu.

Kwa upande wao, Barcelona waliobanduliwa mapema katika Kundi E kwenye Klabu Bingwa Ulaya (UEFA), watakwaruzana na Napoli ya Italia.

Rangers walikamilisha kampeni za Kundi A katika nafasi ya pili kwa alama nane, nane zaidi nyuma ya Olympique Lyon ya Ufaransa.

Dortmund wanaoshikilia nafasi ya pili nyuma ya Bayern Munich kwenye Ligi Kuu ya Ujerumani, walishuka hadi Europa League baada ya kuambulia nafasi ya tatu katika Kundi C kwenye UEFA.

Mechi za mkondo wa kwanza zitatandazwa mnamo Februari 17, 2022 huku marudiano yakifanyika wiki moja baadaye.

Mfumo mpya wa Europa League msimu huu unashuhudia timu nane zilizotawala vilele vya makundi, ikiwemo West Ham United, Lyon na AS Monaco, zikifuzu moja kwa moja kwa raundi ya 16-bora. Vikosi vingine vilivyoingia hatua ya 16-bora moja kwa moja ni Spartak Moscow, Frankfurt, Galatasaray, Red Star Belgrade na Bayer Leverkusen.

Rangers walikutana na Dortmund mara ya mwisho katika raundi ya tatu ya Uefa Cup mnamo 1999-2000 na Wajerumani wakasonga mbele kupitia penalti baada ya pande zote mbili kushinda 2-0 nyumbani.

Tangu wakati huo, Rangers wameshinda mechi mbili, kuambulia sare mara moja na kupoteza mechi tano dhidi ya mpinzani kutoka Ujerumani.

Japo Rangers waliambulia sare za 2-2 dhidi ya Dortmund kwenye hatua ya makundi ya UEFA mnamo 1995-96, walishinda miamba hao wa Ujerumani kwenye European Cup mnamo 1966-67 na Uefa Cup mnamo 1982-83.

Chini ya kocha Marco Rose aliyeagana na Borussia Monchengladbach ya Ujerumani msimu jana, Dortmund walikosa kusonga mbele kwenye UEFA msimu huu kutokana na uchache wa mabao. Walijizolea alama tisa sawa na Sporting Lisbon ya Ureno katika Kundi C lililotamalakiwa na Ajax ya Uholanzi kwa pointi 18.

DROO YA MCHUJO WA EUROPA LEAGUE:

Sevilla vs Dinamo Zagreb

Atalanta vs Olympiakos

RB Leipzig vs Real Sociedad

Barcelona vs Napoli

Zenit St Petersburg vs Real Betis

Borussia Dortmund vs Rangers

Sheriff Tiraspol vs Braga

FC Porto vs Lazio

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Droo ya Klabu Bingwa Ulaya hatua ya 16-bora kufanywa upya...

Barcelona washuka zaidi ligini baada ya kukabwa koo na...

T L