• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 7:50 AM
Wakenya watawala Pittsburgh Half Marathon

Wakenya watawala Pittsburgh Half Marathon

NA GEOFFREY ANENE

WESLEY Kiptoo na Caroline Rotich waliibuka washindi wa mbio za Pittsburgh Half Marathon zilizokuwa zikirejea baada ya kutofanyika 2020 na 2021 nchini Amerika, Jumapili.

Kiptoo alitwaa taji la wanaume kwa saa 1:01:25 akifuatiwa na Mkenya mwenzake James Ngandu (1:01:27) na Mwamerika Jared Ward (1:03:37).

Bingwa wa New York Marathon 2011 na 2013 Rotich, ambaye pia anajivunia taji la Boston Marathon 2015, alitawala kitengo cha kinadada kwa saa 1:09:30. Alifuatwa sekunde 26 baadaye na mzawa wa Kenya Aliphine Tuliamuk (1:09:54) na Mwamerika mwenzake Sarah Sellers (1:11:51).

Muda ya Kiptoo na Rotich ni rekodi mpya ya Pittsburgh Half Marathon. Kiptoo alifuta rekodi ya 1:01:53 iliyowekwa na Leonard Korir mwaka 2019 naye Rotich aliweka rekodi mpya ya kinadada. Alifuta 1:10:04 iliyowekwa na Tuliamuk mwaka 2018. Takriban watu 30,000 walishiriki makala haya. Kwingineko, mfalme wa London Marathon mwaka 2011 Emmanuel Mutai na malkia wa Eindhoven Marathon mwaka 2017 Eunice Jeptoo ni baadhi ya watimkaji watajika watakaowania ubingwa wa makala ya kwanza ya Uhuru Classic Nairobi Marathon mnamo Mei 8.

  • Tags

You can share this post!

KIGODA CHA PWANI: Ngoma ya umoja wa kisiasa Pwani imepoa,...

Ulikosea stepu, Ruto amwambia Uhuru

T L