• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 9:55 AM

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Fasili ya lugha kama nyenzo ya kimsingi ya mawasiliano

Na MARY WANGARI KATIKA makala hii, tutaendeleza uchambuzi wa lugha kama kiungo cha kimsingi katika mawasiliano ya binadamu. Lugha ni mfumo wa ishara – Hii inaashiriwa na jinsi maneno katika lugha huhusishwa au kuambatanishwa na hisia, mawazo, vitu, matendo yanayooana kwa njia ya unasibu. Maandishi kwa mfano ni mkusanyiko wa ishara ambao maana yake inaweza […]

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Aina mbalimbali za malipo na dhima yake katika jamii

Na MARY WANGARI TUMEKUWA tukiangazia aina mbalimbali ya malipo yanayotumika katika shughuli mbalimbali za kijamii. Hii leo tutaendeleza mada hiyo kwa kuangazia na kuchambua kwa kina ada hizo mbalimbali jinsi ifuatavyo: Mahari – Ni malipo yanayotolewa ili kuoa mwanamke au kuolewa na mwanamme kuambatana na jamii husika. Mwago – Ni malipo kwa mke wa kwanza […]

Wasanii mashuhuri waliofariki 2020 hivyo kuacha pengo kubwa katika fasihi yakiwemo majukwaa ya utunzi na ulumbi wa mashairi

NA HASSAN MUCHAI MWAKA 2020 tulipoteza watu mashuhuri nchini na mataifa ya kigeni. Jukwaa la ushairi na Kiswahili kwa jumla halikuachwa nyuma. Kuanzia mwanzo wa mwaka 2020, kilikuwa ni kilio baada ya kilio. Tulianza na kifo cha Abdallah Shamte, Ken Walibora, Abdallah Mwasimba, Sudi Kigamba na mwisho Kombo Mataka Salim – Msijumu. ABDALLAH ALI SHAMTE […]

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Dhana na dhima ya malipo na ada mbalimbali katika jamii

Na MARY WANGARI WANAJAMII huhitaji bidhaa na huduma mbalimbali ili kuwawezesha kufanikisha mambo, kukidhi haja na kuendeleza shughuli za maisha ya kila siku. Ili kupata bidhaa na huduma mbalimbali aghalabu mtu hutakiwa kulipia malipo au ukipenda ada fulani. Katika makala ya leo, tutaangazia kwa kina na kufafanua kuhusu dhana ya malipo almaarufu ada, aina mbalimbali […]

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Umilisi wa usemaji kama kitengo cha uamilifu katika lugha

Na MARY WANGARI MSOMI Chomsky ambaye ni mwasisi wa nadharia ya umilisi wa kiisimu katika lugha anahoji kwamba ni sharti mwanafunzi wa lugha awe na uwezo wa kutumia lugha ipasavyo kando na kufahamu kanuni za lugha husika. Hata hivyo, mwanaisimu Hymes (1971) anataja mtazamo wa Chomsky kuhusu umilisi wa lugha kama ulio finyu akihoji kwamba […]

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Umilisi wa mawasiliano na dhima yake katika kujifunza lugha ya Kiswahili

Na MARY WANGARI KUFAHAMU kuhusu umilisi wa kiisimu katika lugha ya Kiswahili husaidia kuelewa matatizo yanayowakumba wakufunzi na wanafunzi wa lugha katika mchakato wa ujifunzaji lugha na pia jinsi ya kusuluhisha matatizo hayo. Kwa mujibu wa Canale na Swain (1980) umilisi wa lugha hutekeleza majukumu anuai huku mtaalam Stern (1983) akiunga mkono kauli hiyo kwa […]

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Umuhimu wa kuzingatia saikolojia unapotunga fasihi

Na CHRIS ADUNGO JINSI ilivyo katika sanaa nyinginezo, mvuto ni kitu cha kimsingi sana katika fasihi. Kipengele hiki cha mvuto ni muhimu zaidi katika fasihi ya watoto na vijana. Kwa mantiki hii, ili mwandishi aweze kufanikiwa kuiteka saikolojia ya watoto na vijana katika kazi yake ni lazima ahakikishe kazi hiyo inakora saikolojia, masikio na macho […]

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Umuhimu wa majaribio, mitihani katika kuimarisha umilisi wa kiisimu kwa wanafunzi

Na MARY WANGARI ILI mwanafunzi aweze kuwa na umilisi wa kiisimu katika lugha ya Kiswahili, ni sharti aambatishe matumizi ya lugha katika usemi na katika maandishi pamoja na kujifahamisha kuhusu kanuni za kisarufi katika lugha ya Kiswahili. Kwa mujibu wa mwanaisimu Leihman (2006), umilisi wa kiisimu katika lugha yoyote ile huambatanishwa na matumizi yake katika […]

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Viambajengo muhimu katika nadharia ya umilisi wa kiisimu

Na MARY WANGARI KADRI mwanafunzi anavyozidi kusoma na kujiendeleza kielimu ndivyo kuimarika au kushuka kwa kiwango chake cha umilisi wa lugha kinapozidi kuonekana. Kiambajengo cha pili ni kuwa, umilisi wa kiisimu huhusishwa na mtu binafsi anayemiliki lugha. Kila mtumiaji wa lugha husheheni umilisi wa kiisimu wa kipekee ambao ni tofauti na mwenzake. Mwanaisimu Lehmann anafafanua […]

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Ubantu na Uarabu wa Vivumishi vya idadi

Na CHRIS ADUNGO INGAWA nadharia pekee inayosomeshwa vyuoni ni kwamba Kiswahili ni Kibantu kwa asili na kwa dhati yake, bado kuna hoja inayosema kwamba asili ya lugha hii ya upwa wa Afrika Mashariki ni mchanganyiko. Mchanganyiko kwa sababu kunazo nadharia kadhaa zinazotetea chimbuko na asili ya Kiswahili kama lugha chotara au iliyotokana na Kiarabu. Kiswahili […]

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Umuhimu wa tafiti kuhusu umilisi wa lugha katika ufundishaji wa Kiswahili

Na MARY WANGARI KWA mujibu wa Mcmanara (2000), mitihani ya umilisi wa mawasiliano inafaa kupima uwezo wa mzungumzaji katika kiwango cha kanuni za lugha na vilevile katika kiwango cha uamilifu wa lugha. Umilisi wa kiisimu haumaanishi kuwa mzungumzaji ana umilisi wa kutosha katika mawasiliano, hata hivyo. Ni dhahiri kuwa mitihani mingi ya umilisi wa mawasiliano […]