• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:55 AM

FASIHI SIMULIZI: Fasili, sifa, dhima na aina za ngomezi

Ngomezi ni nini? (alama 2) Ni sanaa/fasihi inayotumia ala za kimuziki kuwasilisha ujumbe kwa hadhira au jamii. Fafanua sifa zozote tano za ngomezi (alama 5) Hutumia midundo mbalimbali ya ngoma/ala za muziki. Huhitaji mtaalam wa ngoma. Maana ya midundo mbalimbali hubadilika kutoka kwa jamii moja hadi nyingine. Ni vigumu kwa mgeni au jamii hasimu kutambua […]

Serikali yabuni njia ya kujua vitabu feki, vitabu vipya vya Fasihi vyatoka

Na FAITH NYAMAI WAZAZI sasa watakuwa na uwezo wa kubaini vitabu feki wanapoelekea madukani kuwanunulia watoto wao vitabu vipya vinavyohitajika kwa masomo mbalimbali shuleni. Hii ni kupitia kutuma nambari iliyoko kwenye kitabu walichonunua kwa nambari 22776 kwa simu ya mkononi. Lengo la huduma hiyo ambayo imekumbatiwa na wizara ya elimu ni kuhakikisha kuwa shule, wazazi […]

FASIHI SIMULIZI: Utanzu wa Semi na vipera vyake

MPENDWA msomaji, leo tutagusia utanzu wa Semi. Semi ni tungo fupi zinazowasilisha ujumbe kwa kufumba au kuchora picha ili kutoa ushauri kwa wanajamii. Pia huitwa tungo fupi. VIPERA VYA SEMI Misemo Ni fungu la maneno machache linalobeba maana fiche. Hususan huunganisha dhana mbili kuwa moja? Mfano wa misemo: i) Arusi ya mzofafa – arusi iliyojaa […]

FASIHI SIMULIZI: Tathmini ya kipera cha Miviga katika utanzu wa Maigizo

Na KIPKOROS BORWO ALHAMISI hii, tunaendelea kuangazia kitanzu cha miviga. Tutataja tu, japo kwa akali aina zaidi za miviga, umuhimu wake na changamoto zake kwa jamii. Aina nyingine za miviga: i) Sherehe za kuzaliwa kwa watoto, kwa mfano, kuzaliwa Yesu (Krismasi kwa waumini Wakristo) iliyofurahiwa 25/12/21 ii) Sherehe za kuwapa watoto majina iii) Kuapishwa kwa […]

UCHAMBUZI WA FASIHI: Wahusika, maudhui na vitushi: Sura ya Sita ya Chozi la Heri

Na JOYCE NEKESA JUMA lililopita tuliangazia sura ya tano ya riwaya ya Chozi la Heri. Umuhimu wa mandhari ya msitu wa Mamba uliangaziwa ambapo tuliona jinsi mandhari yalivyochangia kujenga maudhui, wahusika na ploti. Leo tunaangazia sura ya sita ambapo mandhari ni katika shule ya Tangamano. Wahusika wanaorejelewa hapa ni Umulkheri, Mwalimu Dhahabu, Lunga, Naomi, Sally, […]

Hasira orodha ya mwisho ya kuwania tuzo ya fasihi ya Kiswahili ikijumuisha Watanzania pekee

Na MARY WANGARI HISIA kali zimeibuka baada ya orodha ya mwisho ya washindi katika tuzo ya uandishi wa fasihi ya Kiswahili kujumuisha Watanzania pekee. Licha ya jopo la majaji kupokea jumla ya mawasilisho 256 kutoka kwa waandishi mbalimbali kote duniani ikiwemo Kenya, ni waandishi kutoka Tanzania pekee walioteuliwa katika tuzo hiyo ya Mabati-Cornell Kiswahili Prize […]

SAUTI YA MKEREKETWA: Wizara sasa ifanye uamuzi imara kuhusu vitabu teule vya fasihi

Na HENRY INDINDI MOJA katika mambo yaliyozua mijadala mikali katika siku za hivi majuzi ni kusuasua kwa uamuzi kuhusu kuteuliwa kwa ama ‘Nguu za Jadi’ au ‘Paradiso’ miongoni mwa vitabu vingine vilivyoteuliwa vya fasihi. Yamkini, kulikosekana uwazi katika uamuzi uliofanyika na kusema la haki kufikia sasa, walimu wananunua chochote katika vitabu hivi kwa matumaini ya […]

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Jinsi ya kuandaa ratiba ya kudurusu nyumbani na umuhimu wake

Na MARY WANGARI MASOMO kama vile Hisabati, Fizikia, Kemia na Bayolojia huhitaji kufanyiwa mazoezi ya mara kwa mara kuhusu fomula na kanuni kuu muhimu hivyo basi hakikisha unatenga muda wa kutosha ili kufanya mazoezi ya kutosha. Wakati – Panga masomo kwenye ratiba yako kwa kuzingatia uzito wa somo husika. Masomo ya sayansi kama vile Hisabati, […]

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Ratiba ya kudurusu nyumbani kwa wanafunzi

Na MARY WANGARI KATIKA makala iliyopita, tuliangazia kuhusu vigezo muhimu vya kuzingatia wakati mwanafunzi anapounda ratiba ya kusomea nyumbani wakati wa likizo au mapumziko yoyote. Kando ni kwamba wakati wa likizo hutoa fursa muhimu ya mapumziko kwa wanafunzi, umuhimu wa kuwa na ratiba ya kuwezesha kudurusu nyumbani hauwezi ukasisitizwa vya kutosha. Mwanafunzi yeyote anayetaka kutia […]

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Vigezo muhimu katika kutathmini insha-2

Na ENOCK NYARIKI KATIKA makala yaliyotangulia, tulianza kuangazia vigezo muhimu vinavyotumiwa katika utathmini wa insha za wanafunzi katika mtihani. Tulieleza kwamba ni muhimu wanafunzi kuvifahamu vigezo hivi kama njia moja ya kuyajua matarajio ya watahini na kujiandaa vyema ili kuyakidhi matarajio hayo. Tuliangazia maudhui, mtindo na muundo katika muktadha wa insha. Tulifafanua kwamba maudhui ni […]

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Sifa bainifu za lugha kama kiambajengo muhimu cha mawasiliano

Na MARY WANGARI JINSI tulivyokwisha eleza, lugha ni kiungo muhimu kinachotumiwa na binadamu katika karibu shughuli zao zote za kimaisha. Bila shaka nafasi ya lugha kama nyenzo kuu ya mawasiliano kwa binadamu haiwezi ikasisitizwa vya kutosha. Lugha ni mfumo – Mfumo wa lugha una maana kwamba lugha inahusisha vipashio muhimu anuai. Vipashio au viambajengo vya […]