• Nairobi
  • Last Updated April 16th, 2024 6:55 PM
MIKIMBIO YA SIASA: Juhudi za Raila kukomboa Jubilee zinaweza zisifaulu

MIKIMBIO YA SIASA: Juhudi za Raila kukomboa Jubilee zinaweza zisifaulu

Japo Bw Kioni na wenzake waliotimuliwa walipata afueni ya muda kufuatia hatua ya Jopo la Kutatua Mizozo ya Vyama vya Kisiasa (PPDT) kusitisha mapinduzi hayo hadi maombi ya walalishi yatakaposikizwa Februari 24, dalili zaonyesha kuwa hawatafaulu.

“Bw Kioni na wandani wake wa Azimio wakiongozwa na Raila waelewe kwamba Rais Ruto ameapa kutwaa Jubilee. Hii ndio maana afisi ya msajili wa vyama vya kisiasa imeidhinisha kutimuliwa kwake. Jopo la PPDT pia itatupilia mbali malalamishi ya Kioni kwa sababu asasi hiyo ni mojawapo ya asasi huru za serikali ambazo zimetekwa na serikali na sasa zinatekelezwa matakwa yake,” anasema mchanganuzi wa masuala ya kisiasa Martin Andati.

Anatoa mfano wa Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP) ambayo tangu Rais Ruto alipoingia mamlakani imeondoa kesi zilizowakumba baadhi ya wandani wa kiongozi huyo wa kitaifa.

“Jubilee itatwaliwa na mrengo wa Kenya Kwanza kwa urahisi kwa sababu Uhuru anatarajiwa kiondoa kama kiongozi na hatakuwa na ushawishi wowote katika chama hicho hata akisalia kuwa mwanacha mwa kawaida,” anaongeza.

  • Tags

You can share this post!

JUNGU KUU: CASs: Ruto aiga Uhuru kuwatunuku wandani

KIGODA CHA PWANI: Kaunti za Pwani zaweza kujikimu bila...

T L