• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 12:09 PM
Pasta amezea mate kiti cha Wetang’ula

Pasta amezea mate kiti cha Wetang’ula

NA BRIAN OJAMAA

MHUBIRI katika Kaunti ya Bungoma, ambaye pia ni afisa wa chama cha kitaifa cha wafanyabiashara na viwanda Kenya (KNCCI) tawi la Bungoma, Padre Herman Kasili, amejiunga na siasa akimezea mate kiti cha useneta kinachoshikiliwa na Moses Wetang’ula.

Padri Kasili amesema atawania kiti hicho kwa tikiti ya chama cha United Democratic Party (UDP) kinachoongozwa na aliyekuwa mbunge wa Lugari, Cyrus Jirongo.

Mhubiri huyo atashindana na naibu gavana wa Bungoma Profesa Charles Ngome wa chama cha DAP-K, Lawrence Sifuna wa ODM, Jacob Machacha na Bw Wetang’ula anayetetea kiti hicho.

Padre Kasili anasimamia kanisa la Gospel Lighthouse Church Webuye.

Katibu wa Muungano wa vyama vya wafanyakazi nchini (COTU) Francis Atwoli ameunga mkono hatua ya Padri Kasili ya kujitosa katika kinyang’anyiro cha useneta cha Bungoma.

“Binafsi ninampongeza Padri Kasili kwa kujitosa katika kinyang’anyiro cha kumuondoa Wetang’ula kutoka kiti cha useneta kaunti ya Bungoma. Tutamsaidia katika safari hii,” akasema Bw Atwoli.

  • Tags

You can share this post!

Mbunge ashinikiza Naibu Rais ajiuzulu

Ruto aenda kinyume na ahadi ya mahasla

T L