• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 9:48 PM
Damaris Nyiva ‘Minam’: Mwalimu na mwigizaji mahiri

Damaris Nyiva ‘Minam’: Mwalimu na mwigizaji mahiri

NA JOHN KIMWERE

NI miongoni mwa wanawake ambao licha ya kuwa ndio mwanzo wameanza kupiga ngoma wamepania kutinga upeo wa kimataifa pia waigizaji tajika miaka ijayo.

Miaka ya sasa tunazidi kushuhudia waigizaji chipukizi wakiendelea kujitokeza na kujiunga na tasnia ya maigizo kinyume na ilivyokuwa miaka iliyopita.

Ingawa alivutiwa na uigizaji tangu akiwa mwanafunzi wa shule ya msingi, alianza kushiriki filamu mwaka 2019 chini ya kundi la KS Media Production.

“Kusema ukweli nilijikuta kwenye uigizaji wakati ugonjwa wa corona ulitua nchini baada ya shule kufungwa,” Damaris Nyiva Mwaka maarufu Minam anaambia safu hii na kuongeza kuwa amehitimu kama mwalimu wa shule za msingi.

Dada huyu mwenye umri wa miaka 28 pia ni mtaalamu wa masuala ya teknolojia (ICT).

Amekuwa akifunza shule jijini Nairobi ndani ya kipindi cha miaka mitatu sasa.

Binti huyu anasema alipata motisha ya kushiriki filamu baada ya kutazama kazi yake msanii Jackie Agyemang Appiah raia wa Canada na mzawa wa Ghana.

Kisura huyu pia amefanya kazi ya uigizaji na Samsphine Films Production chini ya produsa Sammy Karey Waweru.

Ndani ya kampuni hizo mbili ameshiriki filamu kadhaa zilizopakiwa kwenye mtandao wa YouTube. Filamu hizi zikiwa: ‘Wendo wa Kamuti’, ‘Young Heart’ na ‘Love and Deception’.

”Kiukweli ninapenda kuigiza ambapo ndani ya miaka mitano ijayo ninatamani kuwa mbali kwa sababu ninaamini ninatosha mboga,” akasema.

Pia kafunguka kuwa amepania kushiriki filamu nyingi tu na waigizaji mbali mbali ndani na nje ya taifa hili.

Katika ulingo wa uigizaji barani Afrika angependa kufanya kazi na Nadia Buhari mzawa wa Ghana ambaye ameshiriki filamu kama ‘Eyes of My Husband’, ‘Heart of Men’, ‘Holding Hope’ na ‘Chelsea’ kati ya nyingi nyinginezo.

Anadokeza kwamba anatamani sana kuona kazi zake zimepata mpenyo kupeperushwa kwenye vyombo vya habari.

Kama ilivyo kawaida kwa wasanii wengi nchini anatoa wito kwa serikali iwapige jeki kupaisha sekta ya uigizaji ili kutoa ajira kwa waigizaji wengi wanaoendelea kujitosa kwenye ulingo huo kwenye juhudi za kusaka riziki.

Damaris Nyiva Mwaka maarufu Minam. PICHA | JOHN KIMWERE

Anasema uigizaji ni ajira kama nyingine. Licha ya kuwa ni msanii chipukizi sio mchoyo wa mawaidha. Anashauri wenzie kuwa wajitume na kuomba Maulana awafungulie njia kupata ajira. Pia anawaeleza kuwa kamwe wasigomee talanta zao bali wapambane mwanzo mwisho wakiamia kuwa ipo siku watakumbalika.

Anadokeza kuwa amewahi kuwa katika mahusiano ndani ya miaka mitano lakini baadaye aliichia kuvunjika moyo baada ya kukosana na kila mmoja kushika zake tano. Anasema binfasi alikuwa amejipa kwa mpenziwe akiaminia angekuwa bwanake wa maisha.

Katika mpango mzima anashikilia kuwa anapania kumiliki brandi ya kuzalisha filamu miaka ijayo lengo kuu likiwa kusaidia waigizaji wanaoibukia.

  • Tags

You can share this post!

TUSIJE TUKASAHAU: Rais alikariri kuwa hatakubali hata inchi...

Wapinzani wa Nassir walia serikali ya Joho inawatesa

T L