• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 8:50 AM
Jaji mkuu kuapisha majaji sita endapo Rais Uhuru Kenyatta hatawaapisha katika muda wa siku 14

Jaji mkuu kuapisha majaji sita endapo Rais Uhuru Kenyatta hatawaapisha katika muda wa siku 14

Na RICHARD MUNGUTI

MVUTANO kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Idara ya Mahakama kuhusu uteuzi wa majaji sita wa mahakama ya rufaa na mahakama kuu ulichukua mwelekeo mpya jana huku akipewa siku 14 kuwaapisha.

Asipowaapisha majaji hao sita katika siku hizo 14 basi Jaji Mkuu Martha Koome na tume ya huduma za mahakama JSC wametwikwa jukumu la kuwaapisha ili waanze kazi mara moja pasi kumshirikisha tena Rais Kenyatta.

“Baada ya siku 14 kukamilika na Rais Kenyatta hatakuwa amewaapisha majaji hawa sita basi Jaji Koome na JSC wachukue hatua ifaayo ya kuwapisha majaji hao ili waanze kutekeleza kazi zao mara moja,”waliagiza majaji George Dulu , William Musyoka na James Wakiaga.

Majaji hao walisema tangu 2019 Rais Kenyatta hakuwaapisha baada ya kuteuliwa na JSC kwa mujibu wa sheria.

uya” katika muda wa siku

Wawili kati ya majaji hao sita Joel Ngugi na George Odunga walikuwa miongoni mwa majaji watano walioangusha BBI. Uamuzi huu ni dhihirisho wazi Rais Kenyatta ameshindwa nguvu katika mvutano huu wa kupimana nguvu kati ya afisi ya rais na idara ya mahakama.

Jaji George Odunga…Picha/RICHARD MUNGUTI

Idara hizi mbili ni mojawapo ya asasi tatu zinazounda serikali. Wakitoa agizo kuhusu hatma ya majaji hao sita, Majaji George Dulu, William Musyoka na James Wakiaga walisema itachukuliwa “Rais Kenyatta ameshindwa kutekeleza majukumu yake ya kikatiba ya kuwaapisha majaji hao sita aliochelea kuwateua na kuwaapisha tangu 2019.”

Majaji Dulu, Musyoka na Wakiaga walisema imebidi mahakama itoe maagizo hayo kwa vile Katiba haijatoa mwelekeo hatua itakayochukuliwa dhidi ya Rais “akikaidi na kukataa kutekeleza majukumu aliyopewa na Katiba.”

Majaji hao walisema siku 14 zikipita bila ya Rais Kenyatta kuwaapisha majaji hao sita basi “itaeleweka hana mamlaka tena kutenda majukumu yake na mamlaka zimeyoyoma.”Majaji hao sita ambao Rais Kenyatta alikataa kuwaapisha ni George Odunga, Aggrey Muchelule, Joel Ngugi na Weldon Korir walioteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufaa.

Wengine ni Bw Evans Makori na  naibu wa msajili wa mahakama kuu Bi Judith Omange.  Makori na Omange waliteuliwa na JSC kuwa Majaji katika idara ya Masuala ya Ardhi na Mazingira. Majaji hawa sita walikuwa miongoni mwa majaji 41 walioteuliwa 2019 kisha Rais Kenyatta akachelea kuwateua akidai baadhi yao walihusika na ufisadi.

Majaji Dulu , Musyoka na Wakiaga walisema kuzembea kwa Rais Kenyatta kutekeleza majukumu yake kumepelekea watoe maagizo hayo. Kesi hii ya kuwapa mamlaka Jaji Mkuu na JSC kuwapisha majaji hao iliwasilishwa na  walalamishi kadhaa miongoni mwao wakili Adrian Kamotho.

Walalamishi walisema Rais Kenyatta amekaidi kutekeleza majukumu yake ya kikatiba. Kama adhabu , majaji hao waliamuru afisi ya Rais ilipe gharama ya kesi hiyo. Majaji hao walitupilia mbali ombi la mwanasheria mkuu Paul Kihara Kariuki wasitishe kesi hiyo ya majaji hao sita kusubiri uamuzi wa Mahakama  ya Rufaa.

Bw Kihara alikata rufaa kupinga uamuzi wa majaji watano waliomwamuru Rais Kenyatta awaapishe majaji hao. Baada ya kuteuliwa na kuapishwa kwa Jaji Martha Koome kuwa Jaji Mkuu watatu kuchukua mahala pa Jaji Mkuu aliyestaafu David Maranga,Rais Kenyatta aliwaapisha majaji 34 na kuwaacha hawa sita.

Kupitia kwa wakili Danstan Omari majaji hao walishtaki serikali wakidai walikuwa wamebaguliwa.Jana walipata afueni mahakama ilipoamuru rais awaapishe. Na wakati huo huo Bw Kihara aliponea chupuchupu kutangazwa kuwa hafai kuhudumu katika wadhifa wa Mwanasheria mkuu (AG) kutokana na ushauri anaotoa kwa Serikali na haswa Rais kuhusu                                                                                          suala hili la uteuzi wa majaji 41.

Mwanasheria mkuu ndiye utoa ushauri kwa serikali katika masuala yote. Walalamishi kuhusu uteuzi huu wa majaji sita waliomba mahakama imtimue kazini Bw Kariuki kwa ushauri anaotoa duni na uliopotoka kwa rais.

Mmoja wa majaji 41 waliokuwa wameteuliwa aliaga kukasalia 40.Uamuzi huu wa jana umeonyesha wazi kabisa Rais Kenyatta ameshindwa katika vita hivi vya nivute nikuvute vya uteuzi wa majaji hao kwa vile wataanza kutekeleza majukumu yao pasi kuidhinishwa na rais.

  • Tags

You can share this post!

KAMAU: Uchawi: Tamaduni za jadi zinadunisha jamii

KINYUA BIN KING’ORI: Tumakinike tusichochee ghasia...

T L