• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 9:48 PM
Walioathirika kutokana na kero ya nzige wanaendelea kupata msaada wa chakula

Walioathirika kutokana na kero ya nzige wanaendelea kupata msaada wa chakula

Na SAMMY WAWERU

SERIKALI inaendelea kutoa msaada wa chakula na mahitaji mengine muhimu ya kimsingi kwa familia zilizoathirika kufuatia kero ya uvamizi wa nzige.

Zaidi ya kaunti 32 zilikumbwa na nzige 2019 na 2020, maeneo kame yakiathirika pakubwa. Wadudu hao walishambulia mimea, mazao shambani na malisho ya mifugo, jamii zinazoishi maeneo yaliyoathirika zikikadiria hasara.

“Tunaendelea kutoa msaada wa chakula na mahitaji mengine muhimu ya kimsingi kwa walioathirika,” Katibu katika Wizara ya Kilimo, Mifugo na Samaki Prof. Boga Hamadi akaambia Taifa Leo Dijitali kupitia mahojiano ya kipekee jijini Nairobi.

Prof. Boga hata hivyo hakufichua idadi ya familia zilizoathirika kufuatia kero ya nzige. Mengi ya maeneo yaliyovamiwa na nzige yakiwa yale kame, yanaendelea kuhangaishwa na kiangazi, mifugo wakiripotiwa kufariki.

Zaidi ya kaunti 32 zilivamiwa na nzige. Serikali imethibitisha kufanikiwa kukabili kikamilifu wadudu hao waharibifu.

Katibu katika Wizara ya Kilimo, Mifugo na Samaki Prof. Boga Hamadi asema serikali inaziwapa chakula familia zilizoathirika kutokana na kero ya nzige waharibifu…Picha/ SAMMY WAWERU
  • Tags

You can share this post!

KOMBE LA DUNIA: Raphinha abeba Brazil dhidi ya Uruguay

Kiunjuri aonekana kuasi Ruto na kujiunga na...

T L