• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 9:48 PM
Kaunti kusaidia manesi wanaotaka kwenda ulaya

Kaunti kusaidia manesi wanaotaka kwenda ulaya

Na Alex Njeru

SERIKALI ya Kaunti ya Tharaka Nithi itasaidia kuandaa stakabadhi za wauguzi wanaotaka kwenda kufanya kazi Uingereza kupitia mkataba uliotiwa saini kati ya Kenya na serikali ya UK mnamo Julai mwaka huu.

Akizungumza jana katika hafla ya mazishi katika kijiji cha Mutindwa wa Mbogori, eneobunge la Maara, Gavana Njuki alisema kaunti hiyo ina manesi wengi zaidi kushinda nafasi zilizopo za kazi.nAlisema manesi hao, hasa wanaofanya kazi katika vituo vya afya vya kibinafsi hulipwa mishahara duni kuanzia Sh25,000 ikilinganishwa na wenzao walioajiriwa na serikali ya kaunti kati ya Sh75,000 na Sh100,000.

“Kama serikali ya kaunti kwa ushirikiano na washiriki wengine tuko tayari kuwasaidia wauguzi wengine wanaotaka kufanya kazi hizo Uingereza,” alisema Gavana Njuki. Alisema wafanyakazi hao wa afya watakaosafiri, kando na kupata mishahara itakayowawezesha kujikuza, pia watapata ujuzi wa kiwango cha juu.

Kiongozi huyo wa kaunti alisema kutokana na aina ya kazi inayofanywa na manesi, huwa wanalipwa mishahara mikubwa na wanasakwa mno kote duniani. Katika juhudi za kuboresha maslahi ya wafanyakazi watakaohamia ugenini ulaya, Kenya inalenga kuwatuma wauguzi 20,000 Uingereza kufidia uhaba wa manesi 62,000 nchini humo.

Nchini Uingereza, manesi wanatarajiwa kupata zaidi ya kiasi maradufu cha mishahara ambayo huwa wanapokea kutoka kwa waajiri Kenya.

You can share this post!

Chanjo ya kuzuia corona yaharibika

Raila Odinga atangaza rasmi kuwania urais 2022

T L