• Nairobi
  • Last Updated February 25th, 2024 11:30 AM
Si kila mwasho ukeni husababishwa na kuambukizwa magonjwa ya zinaa

Si kila mwasho ukeni husababishwa na kuambukizwa magonjwa ya zinaa

NA PAULINE ONGAJI

WANAWAKE wengi huingiwa na wasiwasi wanapoanza kushuhudia mwasho ukeni siku kadhaa baada ya kushiriki tendo la kujamiiana.

Kunao ambao wazo linalowajia ni kwamba wameambukizwa maradhi ya zinaa, suala ambalo huenda likawafanya kuwashambulia wapenzi wao. Lakini japo huenda hii ikawa sababu, kuna vichocheo vingine vingi.

Kwanza, huenda mwasho huu unasababishwa na ukavu katika sehemu hii au msuguano mwingi. Ikiwa basi hii ndio sababu, basi mwasho utatokomea baada ya siku kadhaa ikiwa utaepuka tendo la ndoa.

Ikiwa mwasho utaendelea, huenda tatizo hili linatokana na ukavu katika sehemu ya uke, shida ambayo waweza sababishwa na kukaukiwa kutokana na matumizi ya dawa za kihomoni, kwa sababu ya maradhi ya kisukari, au matumizi ya sabuni zilizo na harufu kali.

Pia, huenda hii ikatokana na mzio wa aina fulani ya kondomu au mafuta ya kulainisha uke wakati wa tendo la ndoa. Mwasho pia waweza kuwa kutokana na maambukizi hasa iwapo utaambatana na harufu mbaya, au majimaji yasiyo ya kawaida.

Ikiwa unakumbwa na shida hii, kabla ya kuchukua hatua yoyote ile utalazimika kumuona daktari na ufanyiwe uchunguzi wa kimatibabu ili kubaini iwapo una maambukizi, na hivyo upate tiba.

Ikiwa kuna maambukizi, mwenzako pia atakazimika kutibiwa ili kuzuia maambukizi mapya. Ikiwa uke wako haujalainika vilivyo au unakumbana na ukavu ukeni kutokanana sababu moja au nyingine, unaweza tumia mafuta ya kulainisha uke wakati wa tendo la ndoa.

  • Tags

You can share this post!

Seremala kortini kwa dai la kuchafua mtoto, 12, na...

Milio ya risasi kutulia kwa muda katika Ukanda wa Gaza

T L