• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 9:48 PM
TAHARIRI: Walimu wasihujumu mitihani ya kitaifa wakitafuta ujira bora

TAHARIRI: Walimu wasihujumu mitihani ya kitaifa wakitafuta ujira bora

NA MHARIRI

HABARI za hivi punde kwamba walimu, kupitia vyama vyao vya kitaifa wametishia kufanya mgomo wa kitaifa na hivyo kuvuruga mitihani inayopangiwa kuanza wiki ijayo ni za kusikitisha na kila hatua zinapasa kuchukuliwa kurekebisha hali hiyo.

Kama tulivyowahi kusema kwenye safu hizi, mazungumzo ndio suluhu kwa kila changamoto maishani. Viongozi hao wanapasa kushauriana na Tume ya Kuwaajiri Walimu (TSC) kwa lengo la kutafuta jawabu la kuridhisha pande zote husika.

Ilivyo kwa sasa ni kwamba, Chama cha Walimu Wanaofunza Sekondari na Taasisi za Elimu ya Juu (KUPPET) kimetoa makataa ya siku saba kwa tume hiyo kutimiza matakwa yao kuhusu nyongeza ya mishahara au washiriki mgomo wa kitaifa.

Ni kweli kwamba, baadhi ya maombi ya walimu hao yana msingi ikizingatiwa kwamba, kama wafanyakazi na Wakenya wengine, walimu wameathirika pakubwa kutokana na mfumko wa bei za bidhaa nchini. Hata hivyo kutumia nyongeza hiyo ya mshahara na mgomo wakati huu ambapo mitihani ya kitaifa inakaribia kuanza ili kushinikiza serikali kutekeleza matakwao hayo ni udhalimu mkubwa dhidi ya wanafunzi wasio na hatia.

Walimu wanafahamu fika kwamba, wanafunzi hao hawana uwezo wala wajibu wowote wa kutekeleza katika kufanikisha matakwa yao.

Hivyo basi, tunahimiza pande zote zinazohusika kwenye mzozo huu kuhakikisha hali ya utulivu inadumishwa ili watahiniwa wote wafanye mitihani yao kwenye mandhari ya utulivu bila hofu ya kutatizika kwa vyovyote vile.

Kama walivyodhihirisha viongozi wapya wa Chama cha Kitaifa cha Walimu nchini (KNUT), kuna mengi yanayoweza kuafikiwa kupitia kwa majadiliano badala ya kutumia kifua na migomo ambayo inaathiri wote, wakiwemo wanafunzi wasio kuwa na hatia.

You can share this post!

Raila, Uhuru kupanga ndoa yao upya wikendi

WANDERI KAMAU: Wanaume Afrika wafuate nyayo za Wazungu...

T L