• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 9:48 PM
Lewandowski avunja rekodi nyingine ya ufungaji mabao kambini mwa Bayern

Lewandowski avunja rekodi nyingine ya ufungaji mabao kambini mwa Bayern

Na MASHIRIKA

ROBERT Lewandowski alifunga bao lake la 43 kambini mwa Bayern Munich mwaka huu wa 2021 na kuvunja rekodi ya marehemu Gerd Muller.

Muller aliweka rekodi ya kufunga idadi kubwa zaidi ya magoli katika Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) mnamo 1972 baada ya kutikisa nyavu za wapinzani mara 42.

Lewandowski, 33, alifunga bao mwishoni mwa kipindi cha pili mnamo Ijumaa usiku na kusaidia waajiri wake kukomoa Wolfsburg 4-0 katika gozi la Bundesliga ugani Allianz Arena.

Ushindi huo uliwadumisha Bayern kileleni mwa jedwali kwa alama 43, tisa zaidi mbele ya nambari mbili Borussia Dortmund.

Lewandowski tayari alikuwa amevunja mojawapo ya rekodi za awali za Muller kambini mwa Bayern mnamo Mei 2021 baada ya kupachika wavuni mabao 41 katika kampeni za Bundesliga mnamo 2020-21. Ufanisi huo ulimwezesha kuvunja rekodi hiyo iliyokuwa ikishikiliwa na Muller kwa miaka 49.

Thomas Muller aliyekuwa akinogesha mchuano wake wa 400 katika Bundesliga, aliwafungulia Bayern ukurasa wa mabao katika dakika ya saba kabla ya kuchangia goli la pili lililopachikwa wavuni na Dayot Upamecano.

Leroy Sane alifunga bao la tatu la Bayern kunako dakika ya 59 kabla ya Lewandowski aliyezidiwa ujanja na Lionel Messi kwenye tuzo za Ballon d’Or mnamo Novemba, kuzamisha chombo cha wageni wao na kuweka jina lake kwenye historia ya mabuku ugani Allianz Arena.

Wolfsburg sasa wanashikilia nafasi ya 12 jedwalini kwa pointi 20 sawa na limbukeni VfL Bochum.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Akiri kuiba simu KNH na kutorokea mochari

Kikao kuandaliwa Disemba 20 kujadili mustakabali wa EPL...

T L