• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 9:48 PM
Man-City waangusha Sevilla na kuongeza taji la UEFA Super Cup kabatini mwao

Man-City waangusha Sevilla na kuongeza taji la UEFA Super Cup kabatini mwao

Na MASHIRIKA

MANCHESTER City waliongeza taji la Uefa Super Cup kwa makombe matatu ambayo walijizolea msimu wa 2022-23 baada ya kufunga Sevilla penalti 5-4 kuafuatia sare ya 1-1 mnamo Jumatano jijini Athens, Ugiriki.

Chini ya kocha Pep Guardiola, Man-City walipoteza taji la Community Shield mnamo Agosti 6, 2023 baada ya kufungwa penalti 4-1 na Arsenal kufuatia sare ya 1-1 ugani Wembley, Uingereza.

Wakichezea dhidi ya Sevilla, walipachika wavuni mikwaju yao yote kabla ya Nemanja Gudelj kushuhudia kombora lake likigonga mwamba wa goli.

Awali, miamba hao walilazimika kutoka nyuma na kusawazishiwa na Cole Palmer aliyefuta juhudi za Youssef En-Nesyri aliyewaweka Sevilla kifua mbele.

Sevilla walifuzu kwa kipute hicho cha Super Cup baada ya kuibuka washindi wa Europa League mnamo 2022-23 huku Man-City wakitawazwa wafalme wa Klabu Bingwa Ulaya (UEFA).

Erling Haaland, Julian Alvarez, Mateo Kovacic, Jack Grealish na Kyle Walker walifunga penalti zote za Man-City na kuhakikisha kuwa wanatia kapuni taji la Super Cup baada ya kujizolea pia Kombe la FA na Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo 2022-23.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Gachagua: Kumeza ODM kama Jubilee kutatufanya tuumwe na...

Serikali ya Ruto ni ‘chafu’, serikali za kaunti...

T L