• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 9:48 PM
Uefa yapinga pendekezo la fainali za Kombe la Dunia kuandaliwa kila baada ya miaka miwili

Uefa yapinga pendekezo la fainali za Kombe la Dunia kuandaliwa kila baada ya miaka miwili

Na MASHIRIKA

RAIS wa Shirikisho la Soka la bara Ulaya (Uefa), Aleksander Ceferin, amepinga pendekezo la kuandaliwa kwa fainali za Kombe la Dunia kila baada ya miaka miwili.

Kulingana naye, kutekelezwa kwa pendekezo hilo litayeyusha ladha ya kipute hicho cha haiba kubwa zaidi ulimwenguni.

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limekuwa likifanya utafiti wa kubaini uwezekano wa fainali hizo kwa upande wa wanaume na wanawake kuandaliwa kila baada ya miaka miwili badala ya minne.

Mchakato huo uliokumbatiwa na FIFA baada ya pendekezo la Shirikisho la Soka la Saudi Arabia mnamo Mei 2021, unaoongozwa na kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger. Wenger ndiye mkuu wa kitengo cha makuzi ya soka duniani katika FIFA.

Fainali za Kombe la Dunia kwa wanaume zimekuwa zikiandaliwa kila baada ya miaka minne tangu kipute hicho kianzishwe mnamo 1930. Ni mnamo 1942 na 1946 pekee ambapo utaratibu huo ulikiukwa kutokana na Vita vya Pili vya Dunia.

Kivumbi hicho kimekuwa pia kikiandaliwa kila baada ya miaka minne kwa upande wa wanawake tangu kianzishwe mnamo 1991.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Mkakati wangu ni wa kuleta maendeleo na amani – Ruto

Mifuko ya supa ya Mulei ilikutwa ndani ya nyumba ya afisa...