• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 3:46 PM
Tusker, Gor zalenga ushindi Caf kesho

Tusker, Gor zalenga ushindi Caf kesho

Na CECIL ODONGO

Tusker na Gor Mahia zimesisitiza kuwa zitapigania ushindi katika mechi za mkondo wa kwanza kwenye Kombe la Mashirikisho hapo kesho dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia na AS Otoho d’Oyo ya Jamuhuri ya Congo (Congo Brazzaville mtawalia.

Huku mechi ya Gor ikiwa imeratibiwa kuanza saa 11.30 jioni katika uga wa Alphonse Massemba-Debat jijini Brazzaville, ile ya Tusker itaanza mnamo saa tisa mchana katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo.Kwa kocha wa Tusker Robert Matano, mechi hiyo inampa nafasi murwa ya kuvunja rekodi duni ambayo amekuwa nayo dhidi ya timu za Kaskazini mwa Afrika.

Tangu kuwasili nchini mnamo Alhamisi, wachezaji, benchi ya kiufundi na maafisa walioandamana na timu, idadi yao ikiwa 35, wamekuwa wakiishi katika hoteli ya Serena.Vilevile wamekuwa na vipindi viwili vya mazoezi katika uwanja wa MISC Kasarani Annex.

Hivi leo, Tusker watakuwa wakishiriki mazoezi yao ya mwisho katika uga wa kitaifa wa Nyayo huku CS Sfaxien pia wakiwa ugani humo baadaye jioni.Ingawa kamati ya muda iliyowekwa kusimamia soka nchini chini ya Jaji Aaron Ringera ilisema kuwa mechi hiyo itakuwa wazi kwa mashabiki, mwenyekiti wa Tusker Dan Aduda alisema kuwa Caf haijajibu barua yao ya kutaka mashabiki wahudhurie mechi hiyo na itawapa mashabiki 2,000 pekee wa timu hiyo tiketi ya kuhudhuria ngarambe hiyo.

Baada ya kuaibishwa 5-0 na Zamalek SC katika mechi ya raundi ya kwanza ya Klabu Bingwa Afrika (CAF), Matano jana alieleza Taifa Leo kuwa mara hii wamejiandaa vyema kwa kuwa wakati ule wachezaji wao wapya hawakuwa wakielewana vyema.Hata hivyo, CS Sfaxien ambao ni mabingwa mara mbili wa Kombe la Mashirikisho si rahisi ikizingatiwa kuwa wamekuwa wakitawala soka ya Tunisia.

Ingawa hivyo, ushindi katika mechi ya mkondo wa kwanza utawapa nafuu na nafasi ya kupigana katika mechi ya mkondo wa pili.Gor Mahia ambayo itacheza dhidi ya AS Otoho d’Oyo iliwasili salama salmini Brazzaville na baadaye kupitia vipimo vya virusi vya corona hapo jana.

Timu hiyo inatarajiwa leo itafanya mazoezi ya mwisho katika uga wao kabla ya kuvaana na wapinzani wao hapo kesho. Timu ambayo itashinda mechi hizo za mikondo ya pili, zitafuzu hatua ya makundi ambapo zitapokea ufadhili wa Sh27 milioni kutoka kwa Caf.

You can share this post!

Arteta anataka mzee Wenger arudi Arsenal

Timu 10 kushiri Mini-ligi ya Kaunti ya Taita Taveta wikendi

T L