• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 7:53 PM

Watanzania walemea Wakenya katika tuzo za Fasihi

NA WANDERI KAMAU WATANZANIA waling’aa kwenye mashindano ya 2023 ya Tuzo ya Fasihi ya Safal-Cornell, kwa kuibuka washindi kwenye vitengo vyote. Kwenye mashindano hayo, yaliyofanyika katika hoteli moja, Ijumaa, jijini Nairobi, hakuna Mkenya hata mmoja aliyeibuka mshindi, licha ya baadhi ya waandishi nchini kuwasilisha kazi zao. Mwandalizi mkuu wa mashindano hayo huwa ni Profesa Mukoma […]

Wasanii kutoka Kenya wang’aa kwenye tuzo  

NA CHARLES WASONGA MKENYA Monica Bene Mutumi ni miongoni mwa wanaharakati wa haki za kibinadamu waliotuzwa na shirika moja la kupigania haki, umoja na amani Afrika kwa kutumia sanaa kutetea haki za wanyonge katika jamii. Bi Mutumi, ambaye ni mshairi, alitawazwa mshindi katika kitengo cha Msanii Mwanaharakati wa Mwaka wa 2023 katika tuzo za Africa […]

Mshairi anayeishi na ulemavu wa ngozi ajizolea sifa ndani na nje ya Lamu

NA KALUME KAZUNGU ALIDINDA kabisa kusalia ndani ya nyumba sawa na walemavu wengi ambao mara nyingi huishia kufichwa chumbani kutokana na dhana potovu ya baadhi ya jamii zinazowakandamiza na kuwazuia walemavu hao wasionekane, wakiamini kufanya hivyo ni kuzuia kicheko au aibu. Kutana na Bw Khalid Omar Ali almaarufu ‘Kanjenje’ ambaye ni mlemavu wa ngozi. Licha […]

Malenga akariri mashairi yenye maudhui ya Ramadhani

NA KALUME KAZUNGU KUTANA na Hashim Said Mohamed, almaarufu DJ Fakhrudin,36. Ni malenga aliyejitolea kuupamba msimu wa Ramadhani kisiwani Lamu kila unapowadia kupitia kutunga na kughani mashairi anayotumia kuwatumbuiza wazee, vijana kwa watoto. Tungo zake za mashairi au tenzi ni nakshi tosha kwani huwa zimesheheni beti, mizani na mistari yenye vina tamutamu. Mashairi yake huwa […]

DOUGLAS MUTUA: Kweli Kenya imehalalisha ushoga au ni hisia kali tu?

NA DOUGLAS MUTUA HIVI haramu imehalalishwa, yaani ushoga ukaidhinishwa kisheria nchini Kenya? Hii ninayosikia ni mihemko ya kawaida tu au watu wanakifahamu fika wanachokisema? Tuelewane tangu mwanzo: Binafsi ni mhafidhina, hivyo ninaupinga ushoga – usagaji na ubasha – kwa asilimia zote na sitabadili msimamo huu hadi nifukiwe kaburini. Hata hivyo utaniwia radhi, lazima nikwambie hivi: […]

GWIJI WA WIKI: Dotto Rangimoto

NA CHRIS ADUNGO MWANDISHI asiye na ujuzi wa kutumia lugha kwa ufundi hukosa uhuru wa kusema anachokitaka kwa jinsi anavyotamani kifikie hadhira lengwa. Ingawa uhuru wa mwandishi umo katika utashi na falsafa, lugha ndicho kitovu cha fasihi na kamba inayovuta hadhira kwa dhamira ya sanaa yenyewe. Dotto Daudi Rangimoto anaamini kuwa kigezo cha kubaini mwandishi […]

MALENGA WA WIKI: Zamu leo ni ya msomi maarufu na mshairi kutoka Tanzania

NA HASSAN MUCHAI LEO tumebahatika kumpata mshairi, mhadhiri, mwanafalsafa , mtetezi wa dini na msomi maarufu kutoka taifa jirani la Tanzania. Jina la Profesa Shabaan Yusuf Kibwana Nyagatwa Sengo au kama anavyojulikana na wengi kama Prof Tigiti Sengo si maarufu tu katika vyuo vyote vinavyotoa mafunzo ya lugha ya Kiswahili Afrika Mashariki ila pia nchi […]

MALENGA WA WIKI: Nyakundi ni mshairi na mhariri wa riwaya, tamthilia

NA HASSAN MUCHAI DUKE Nyagwoi Nyakundi almaarufu mwalimu Nyakundi alizaliwa mwaka wa 1994 eneo la Ogembo, katika Kaunti ya Kisii. Ni mtoto wa kwanza miongoni mwa watano wa Bw Enock Ondigi na mama Margaret Nyabonyi. Nyakundi alianza masomo yake katika shule ya Olympic Junior Academy iliyoko Rionyiego, Nyamache. Akiwa shule za msingi na upili alipenda […]

NGUVU ZA HOJA: Tujifunze Kiswahili kutoka kwa wazee mikota wenye tajiriba pevu

NA PROF IRIBE MWANGI JUMATATU nilikuwa na kikao na watu muhimu katika ulimwengu wa Kiswahili. Mmoja wao ni Balozi Wanjohi, Mkurugenzi wa Diplomasia ya Utamaduni katika Wizara ya Maswala ya Kigeni na Dayaspora. Balozi Wanjohi amekuwa mpenzi na shabiki mkubwa wa Kiswahili na kuna matumaini kwamba atasaidia katika usambazaji wa Kiswahili hasa kupitia balozi zetu. […]

MWALIMU WA WIKI: Kwa Akinyi ualimu si kazi bali uraibu hasa!

NA CHRIS ADUNGO ZAIDI ya kuwa na ujuzi wa kufundisha na kipaji cha kutumia vifaa mbalimbali vya ufundishaji, mwalimu bora anastahili kuteka saikolojia ya wanafunzi wake darasani kwa wepesi. Shughuli za ufundishaji zitakuwa rahisi iwapo mwalimu atasikiliza wanafunzi, kuelewa changamoto zao na kuwaelekeza hatua kwa hatua. Hii ni kazi ngumu inayohitaji moyo na subira. Aidha, uhusiano wa karibu kati ya mzazi na mwalimu utafunua mengi […]

Wataalamu na wasomi wa Kiswahili watathmini maendeleo yake nchini

Na CHRIS ADUNGO WARSHA ya Kiswahili iliyofanyika katika ukumbi wa Alliance Française jijini Nairobi mnamo Julai 8, 2022, iliwapa baadhi ya wataalamu wa lugha fursa ya kutathmini hali na maendeleo ya Kiswahili nchini Kenya. Semina hiyo iliandaliwa na Shirika la Twaweza Communications kwa ushirikiano na Idara ya Masomo ya Kiafrika katika Chuo Kikuu cha Yale, […]

MWALIMU WA WIKI: Ni mwalimu mkuu na mwandishi stadi

NA CHRIS ADUNGO ZAIDI ya kufundisha, mwalimu ana wajibu wa kukuza viwango vya ubunifu miongoni mwa wanafunzi wake na kuwaamshia ari ya kuthamini utangamano. Shughuli hizo zitakuwa rahisi iwapo mwalimu atateua kutumia mbinu zitakazompa majukwaa anuwai ya kushirikiana vyema na wanafunzi wake kutalii mazingira mbalimbali, kushiriki masimulizi na kufanya kazi ya usomaji katika vikundi. Kuhusisha […]