• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 8:55 PM

KAULI YA MATUNDURA: Walibora alivyopagazwa wizi wa miswada

Na BITUGI MATUNDURA MAKALA ya mwandishi Ken Walibora ‘Ukarimu wa Wallah katika tasnia pana ya Kiswahili’ (Taifa Leo, Machi 9, 2017) yaliibua kumbukumbu muhimu katika akili yangu. Katika makala hayo, Walibora – ambaye nimewahi kudai kuwa ni mmoja wa waandishi aali wa fasihi ya/kwa Kiswahili Afrika ya Mashariki kuwahi kuonekana mpaka sasa, na katika makala […]

Hospitali yajiondolea lawama kifo cha Walibora

Na CHARLES WASONGA AFISA Mkuu Mtendaji wa Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH) Dkt Evanson Kamuri amekana madai kuwa wahudumu wa hospitali hiyo walimtelekeza mwandishi mahiri Prof Ken Walibora alipofikishwa huko kwa matibabu Aprili 10. Dkt Kamuri akihojiwa Jumatatu amewaelezea wanachama wa Kamati ya Seneti kuhusu Afya hatua kwa hatua jinsi Profesa Walibora alivyopoteza maisha […]

Seneti kuchunguza kifo cha Walibora

Na CHARLES WASONGA BUNGE la Seneti Jumatatu litaanzisha uchunguzi kuhusu kifo cha mwandishi hodari na mwanahabari marehemu Profesa Ken Walibora. Kamati ya Seneti kuhusu Afya imemwagiza Afisa Mkuu Mtendaji wa Hospitali Kuu ya Kenyatta (KNH) Dkt Evans Kamuri kujibu maswali kuhusu madai kuwa Walibora alitelekezwa na wahudumu wa hospitali hiyo alipowahiwa huko baada ya kugongwa […]

Kwaheri Walibora, wengi tutakupeza

Na OSBORNE MANYENGO MWANDISHI mahiri na mwanahabari mbobevu, Prof Ken Walibora hatimaye alizikwa jana nyumbani kwao eneo la Bonde, Suwerwa, kilomita nne kutoka Makutano kwa Ngozi, Cherang’any, Kaunti ya Trans Nzoia. Mwili wa Prof Walibora uliwasili nyumbani kwao saa nane na dakika 26 na kupokelewa kwa majonzi makuu na familia na marafiki, wote kwa jumla […]

Kwaheri Prof Walibora

Na CHRIS ADUNGO ULIMWENGU ni jukwaa la pekee kwetu sote kuigizia tamthilia inayoitwa ‘Maisha’ – mchezo ambao siku zote mwelekezi wake ni Mwenyezi Mungu aliye chanzo cha uhai na vipaji vyote tulivyonavyo. Mchezo huu unajumuisha maonyesho matatu ambayo ni mwanadamu kuzaliwa, kuoa au kuolewa kisha kuaga dunia. Kipindi cha zaidi ya wiki moja na nusu […]

Walibora alitabiri kifo chake

NA MARY WANGARI [email protected] Huku taifa na ulimwengu kwa jumla ukiwa umetikiswa na habari za kutisha kuhusu kifo cha mwandishi nguli Profesa Ken Walibora, imebainika kwamba marehemu huenda alitabiri kuhusu kifo chake miaka mingi iliyopita katika vitabu alivyoandika. Haya yanajiri wakati ambapo kifo cha kutatanisha cha msomi huyo kimesalia kitendawili kigumu hasa kufuatia ripoti ya […]

Utata zaidi ripoti ikiashiria Walibora aliuawa

Na CHRIS ADUNGO POLISI sasa wameshinikizwa kutoa video za kamera za CCTV zitakazosaidia kutegua kitendawili cha kifo cha Prof Ken Walibora. Wakenya mitandaoni jana walisema, video hizo zitatoa majibu ya wakati na jinsi msomi huyo aliyeegesha gari lake katika Barabara ya Kijabe, alivyofika Muthurwa inakodaiwa aligongwa na matatu ya kampuni ya Double M. Inadaiwa Prof […]

Niliposikia kifo cha Walibora, mikono yangu iliganda – Jack Oyoo Sylvester

Na GEOFFREY ANENE Kenya inaendelea kuomboleza kifo cha Profesa Ken Walibora, huku mtangazaji shupavu wa Shirika la Utangazaji Kenya (KBC) Jack Oyoo Sylvester akimkumbuka mwendazake kama mtu aliyependa kabumbu. Jack almaarufu Kaka Jos, ambaye alimuingiza Walibora katika kutangaza mpira miaka 20 iliyopita alipompeleka uwanjani wa mechi ya Ligi Kuu na kumpatia kipazasauti, ameeleza tovuti ya […]

Walibora hakujua kuficha uozo, alieleza yaliokuwa moyoni bila kutetereka – Kennedy Wandera

NA KENNEDY WANDERA Nilikutana na Prof Ken Walibora Juni 22, 2016 saa 8:02 katika makao makuu ya taasisi yaukuzaji mitaala nchini Kenya KICD jijini Nairobi katika juhudi za kupanua na kueneza matumiziya lugha ya Kiswahili ukanda wa Afrika Mashariki. Hapa palikuwapo wataalamu na wanahabari wa Kiswahili. Hapa lengo lilikuwa moja tu: Kuzindua rasmi Chama cha […]

KAULI YA WALIBORA: Korona ni baniani akuzaye msamiati wa Kiswahili

NA PROF KEN WALIBORA KWEMA msomaji wangu mpendwa? Nashukuru sana kwa shauku yako ya kusoma safu hii kila wiki tangu 2016. Kariha yangu ya kuandika inatoka kwako. Miye si bingwa wa masuala ya afya ila nashauri kwa unyenyekevu uendelee kujilinda dhidi ya janga lililotufikia kwa kunawa mikono, kuvaa barakoa, kutowasalimia watu mikononi, kuepuka vikundi vya […]

KAULI YA WALIBORA: Mbona twaogopa kukiuka haki za wauaji wa lugha?

NA PROF KEN WALIBORA HII ni enzi ya uhuru na haki. Katika enzi hii nimeona watoto wa shule za msingi wakiandamana na mabango yenye maneno yanayosema, “Haki yetu” na wakipiga mayowe sawia na maneno hayo. Hii haki inafungamana na ung’amuzi wa uhuru wa msingi. Watu wanawania kuwa huru kwa lolote lile. Na hivi uhuru na […]

KAULI YA WALIBORA: Kuundwa kwa Baraza la Kiswahili njia pekee ya kuenzi wafia lugha

NA PROF KEN WALIBORA SIKU zote alipokuwa bungeni, Kathangu alikuwa akizungumza Kiswahili, japo hakuwa mzawa wa Uswahilini”?Wiki hii namkumbuka mbunge wa zamani wa Runyenjes, Njeru Kathangu. Kwa kizazi kipya cha vijana nchini Kenya huenda hili jina lisiwe na mashiko yoyote. Ni sawa na majina yaliyosahaulika kama vile Naftali Temu, Henry Rono, Ben Jipcho, Elizabeth Onyambu […]